Ok9
JF-Expert Member
- Oct 5, 2013
- 4,549
- 4,133
Ninaandika haya nikiwa na ushahidi wala sio mambo ya kusimuliwa.
Nilipokuwa mdogo, kuna stori za mtaa kwamba Padri flani akikulaani inakupata. Nikawa na wasiwasi juu ya hilo, lakini katika kukua kwangu nikalithibitisha.
1. Padri mmoja alkuwa muda mwingi anatumia kusali. Ilkuwa akitukuta njiani au shuleni anauliza kwanini hujaenda kanisani? Na ikumbukwe hakujui, na ibada zipo 4 na kanisa ni kubwa! Hadi leo ninajiuliza sana uwezo wake.
2. Katika ujenzi wa kanisa hapa Ushirombo, ni miaka ya 90 waljitokeza wafadhil wa Ujerumani katika ujenzi lakini ikaonekana kuna migogoro kwamba wanajenga kwa upendeleo. Iliibua kelele nyingi sana na mwishowe Padre wa Kijerumani akavunja sarafu ya sh 1 mbele ya waumini akasema "Hakuna kanisa hapa", na kweli hadi leo ule mji umechangamka sana lakini hakuna Parokia.
3. Mwaka jana Padri mmoja alifungisha ndoa akasema, "Hii ni ndoa yangu ya kwanza kufungisha, ikitokea mmoja wenu kumwacha mwenzie, na awe mwehu". Leo yule mwanaume ni chizi!
Hebu tujiulize kuna nini kikubwa hapo?