SoC04 Nguvu za kiume, michezo ya kubashiri na sekta ya habari na mawasiliano

SoC04 Nguvu za kiume, michezo ya kubashiri na sekta ya habari na mawasiliano

Tanzania Tuitakayo competition threads

usshindi

Member
Joined
May 14, 2024
Posts
5
Reaction score
10
TANZANIA tuitakayo ni Ile iliyokamilika katika nyanja zote iwe Bora katika afya ya kijamii Ili iweze kufanya shughuli za kimaendeleo.

Ninapenda kuunganisha maneno haya maudhui haya mawili yaliyoshamiri katika jamii kwa Sasa na wizara ya habari na mawasiliano kwa ujumla kwa uhusiano niliouona na nitakaoulezea humu ndani.

Sio jambo geni Tena kwa siku za hivi karibuni hapa nchini Tanzania kukutana na machapisho ya Tiba za nguvu za kiume biashara za dawa za kuongeza uwezo wa ustahimilivu katika tendo la ndoa sio vigumu Tena kukutana na masuala ya michezo ya kubashiri na mambo mengineyo mengi yanayoathiri nguvu kazi katika jamii

Wakati Fulani nikiwa nafanya mawasiliano na rafiki yangu Mmoja kutoka china katika mtandao wa interpals niligundua utofauti uliopo kati ya TANZANIA na China katika uchujaji wa vitu mtandaoni nikapata wazo kua ni jambo zuri kama mchakato huu ukiboreshwa nchini kwetu unaweza kusaidia jamii

Siku hiyo tulikua tulifanya mazungumzo kuhusu games na mitandao ya kijamii rafiki yangu aliwahi kuniambia kuwa China wanazuia mitandao mingi ya kijamii na pia wanaweza kupunguza au kuongeza applications zilizopo kwenye appstore za simu za wakazi wa China. Pia akanielekeza kuwa wanaweza kufuatilia matumizi ya mtandao ya mtu Mmoja Mmoja, nikagundua hili jambo hata Tanzania linaweza kufanyika lakini utofauti wa jambo hili kati ya Tanzania na China linabaki kuwa kwenye ubora, niligundua hili jambo baada ya kumtumia screenshot ya application Moja iliyopo kwenye simu yangu akanijibu kwake haipo na hawezi kuipakua.

Ninarudi hapa nchini kwetu wataalamu wengi wa kiafya kupitia marejeleo mbalimbali wanahusianisha matatizo ya nguvu za kiume na afya ya akili wakisema uwepo wa msongo mwingi kwa vijana au mtu yeyote kunaweza kuathiri nguvu zake za kiume, pia baadhi ya wataalam huhusianisha upungufu wa nguvu za kiume na utazamaji wa video za utupu ambapo wengi wa vijana huishia kujichua na kusababisha ulegevu wa misuli ya uume.

Nikianza na msongo wa mawazo nitauhusianisha na suala la michezo ya kubahatisha.

Serikali ya Tanzania inapata mapato yake kupitia michezo hii ya kubahatisha lakini haipaswi kusahau kuwa kuna vijana wanazidi kuharibika kwenye afya zao za akili kwa sababu ya michezo hii ya kubahatisha. Kama umewahi kushiriki katika michezo hii, serikali zimewekwa sheria na misingi ya mtu kucheza michezo hii ya kubahatisha.

Miongoni mwa sheria hizo ni umri wa mtu kushiriki michezo hiyo kuwa ni miaka kumi na nane na kuendelea lakini sheria hii haifuatiliwi kwa maana vijana wengi waliopo chini ya umri wa miaka kumi na nane wanashiriki mtu yeyote aliyepita katika vituo hivi ni shahidi wa hili vijana wa shule hasa ngazi ya sekondari hua wanashiriki katika michezo hii, jamii inazidi kuathirika watoto wanacheza kwa kutumia ada na pesa muhimu wanaishia kwenye dimbwi la mawazo

Sehemu nyingine ya kucheza michezo hii huwa ni mitandaoni, sheria iliyoko ni umri wa miaka 18 lakini kwa upande wangu ninaona ni suala la kijana kumiliki simu mtu anaecheza kwa kutumia ussd hawezi kuulizwa umri wake Cha ajabu kabisa ni watu wanaochezea mtandaoni wao wanakutana na box la kuweka tick kuthibitisha kuwa ana umri wa miaka 18 hili jambo hata mtoto wa miaka mitatu anaeza kuthibitisha kuwa na umri wa miaka 18.

Serikali iboreshe iunganishe nyaraka muhimu zinazotambulisha umri wa mtu wakati wa kusajili akaunti za kubashiri Ili kukilinda kizazi kisicho sahihi kucheza michezo kutokana na athari zake kama Hilo la nguvu za kiume mamlaka yoyote Ile inayohusika na ufuatiliaji wa suala hili jambo linawezekana na litanusuru kizazi kijacho.

Suala lingine ni maudhui ya picha na sinema za uchi mitandaoni. Serikali imefanya jitihada za kubadili sheria zinazobana upatikanaji wa sinema za utupu mitandaoni lakini mpaka Sasa bado suala halijafanikiwa, hapa ndipo ninaihusisha Wizara ya Habari na Mawasiliano Moja kwa Moja kama Wizara ambayo inaeza kupambana na hili na kufanikisha.

Miongoni mwa sheria zilizotoka miezi ya hivi karibuni na likawashtua wengi ilikuwa kufungia vpn zisizo halali nchini, suala lilileta taharuki kwenye mitandao mingi ya kijamii lakini kwangu mimi hili lilikuwa na mchango mkubwa kwenye kupunguza au kuondoa kabisa upatikanaji wa sinema na picha za utupu mitandaoni

Serikali inapaswa kusajili na kufuatilia kwa ukaribu vpn namna zinavyotoa huduma zake kwa wateja lakini sheria ya kuondoa kabisa VPN zinazoruhusu upatikanaji wa maudhui yasiyohotajika kwenye appstore za nchini Tanzania ndilo jambo la muhimu sana.

Pia uwepo wa mitandao ya kijamii inayotoa urahisi wa upatikanaji wa maudhui hayo kama Twitter (x), telegram, na Facebook unapaswa kupigwa marufuku au kupewa namna nzuri ya kuendesha mitandao yao kwenye nchi yetu Ili kuzuia mianya.

Hilo halitoshi serikali kupitia wataalam wake wa tehama wanapaswa kuzuia advertisement zote zinazotolewa na makampuni mbalimbali mitandao zenye maadili yasiyofaa kwa maana Kuna wakati matumizi ya mitandao yanakosa usalama unapokua karibu na watu wa heshima kwa sababu ya advertisement za picha na video za utupu .

Nguvu za kiume ni afya ya jamii ni nguzo ya afya ya akili ni msingi katika utimizaji wa majukumu katika jamii bila afya ya jamii hakuna maendeleo serikali iweke maanani katika hili.
 
Upvote 4
Serikali iboreshe iunganishe nyaraka muhimu zinazotambulisha umri wa mtu wakati wa kusajili akaunti za kubashiri Ili kukilinda kizazi kisicho sahihi kucheza michezo kutokana na athari zake kama Hilo la nguvu za kiume mamlaka yoyote Ile inayohusika na ufuatiliaji wa suala hili jambo linawezekana na litanusuru kizazi kijacho.
Hii itasaidia sana kuwadhibiti watoto.

Lakini suala kubwa litakuwa mtu binafsi kujidhibiti mwenyewe. Ni kama suala la pombe tu serikali kupiga marufuku haifai, lakini mtu binafsi kujidhibiti ndio mpango

Pia uwepo wa mitandao ya kijamii inayotoa urahisi wa upatikanaji wa maudhui hayo kama Twitter (x), telegram, na Facebook unapaswa kupigwa marufuku au kupewa namna nzuri ya kuendesha mitandao yao kwenye nchi yetu Ili kuzuia mianya.
Kama hapa, pamoja na uwepo wa AI zinazochakata picha. TCRA imefikiria kuweka mfumo utakaozuia picha chafu kisemi-automatic hata??
Tena sio lazima mitandao yote, waweke hata kwenye mitandao ya kijamii tu baaasi
 
Back
Top Bottom