NGUVU ZA SALA.

NGUVU ZA SALA.

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Karibu binti na mwana wa mama Afrika.

Watu hufanya sala kama sehemu ya mazowea ya kuongea na Mungu.

Mbele ya pazia unaongea na Mungu wewe, Nyuma ya pazia unatekeleza mwenyewe.

Unaweza dhani nimejichanganya au nimekuchanya, rejea kauli ya Mungu, mbingu na kila kitu kipo ndani yako.

Ipo hivi.
Kwa lugha halisi kanuni ya kuu za kuwasiliana na Mungu zipo mbili katika moja, nayo ni kuongea na nafsi yako.
Au kutumia wenye au vyenye uwezo mkubwa kiimani kuwasiliana na Mungu kwa niaba yako.
Kwenda kwa mtu fulani akuombee, ni lugha ya kuwa wewe huna imani inayoweza kuleta matokeo.
Naye anarudi katika njia kuu ya kuwasiliana na Mungu yeye kwa niaba yako.

Kiimani kusali ni kuwasiliana na Mungu kiroho, kufikisha haja zako za aina mbalimbali, iwe maombi, majibu, shukrani n.k.
Sala husogezwa mbele za Mungu kwa njia mbili.
Moja kwa maneno.
Mbili kwa mawazo.
Kufumba macho ni kutafuta utulivu wa nafsi.

Wote wenye utaratibu wa kusali, kuna wakati nafsi zao zitakubaliana na akili kuwa sala zao hazijasikilizwa.
Namaanisha kuwa kuna wakati mtu unasali lakini hupati hisia za kusikilizwa, na kuna wakati unapata hisia kabisa kama Mungu kasikia sala yako.

Hali zote hizo zikitokea si kama Mungu muumbaji hajasikia, au amesikia.
Nafsi tatu ndani ya mtu mmoja, unazimiliki wewe, hivyo wewe ndiye muumbaji wa kila kitu katika Dunia.

Wanasaikolojia akina plato, eristote, sokret, wengine wote, kutia ndani Yesu na Mohammad.
Wanakubaliana, kila kitu katika maisha ya mtu kinatokana na mtu mwenyewe.
Ikiwa na maana matukio yanayotutokea katika maisha yetu tumeyapanga wenyewe.
Kama wewe ni maskini, umepanga kuwa hivyo, kama wewe ni tajiri umepanga kuwa hivyo.

Matukio mengine tunayopitia au kukutana nayo katika maisha, kuoa, familia, majirani, watoto, kabila, taifa hivyo ulichagua kabla hujaja Duniani hilo lina somo lake Acha niendelee na somo husika.

Ukiingi katika Maandiko, Mungu aliumba kwa neno, kwa neno kila kitu kilifanyika.

Nimewahi sema kuwa, story nzima ya Maandiko inakuzungumzia wewe.
Hivyo Maandiko yakisema hapo mwanzo palikuwapo neno, naye neno alikuwako kwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwa Mungu na hakuna kilichofanyika pasipo Yeye (yohana 1:1).

Narudia tena Biblia si kitabu cha kihistoria, bali ni masimulizi ya kiroho kwa njia ya visa asili.
Hivyo tunaweza sema biblia ni Tamathali, hivyo inaweza kutumia neno Simba lakini si mala zote wanamaanisha Simba bali kitu au jambo lenye kuendana na Simba.

Ukilitoa hilo fungu katika Tamathali.
Ipo hivi.

Kabla ya mtu kufanya chochote, hicho kitu kinaanzia katika fikra, ambazo zinatafsiriwa kama roho.
Fikra ni nguvu ya kufikiri.
Mfano. Nataka kujenga nyumba, nitaanza kuijenga na kuimaliza kwanza katika mawazo.
Hayo mawazo ndiyo neno ambaye ametokana na roho.
Nikikamilisha ujenzi wa nyumba katika mawazo, ndipo naanza sasa kuiumba ( kuijenga ) hiyo nyumba ili ionekane.
Ikiwa na maana kabla haijaonekana nyumba kidhahiri, ilikuwepo katika mawazo.
Nikianza kuijenga ndiyo mwanzo unaofahamika na watu, kama nimeanza kujenga.
Hivyo biblia ikisema hapo mwanzo palikuwapo neno inamaa, hapo mwanzo ilikuwepo nyumba, na hiyo nyumba ilikuwepo katika mawazo yangu, na bila mawazo yangu isingetokea nyumba.

Kwa mfano huo ukiwaza au kujisemea maneno au mawazo mabaya, yatakutokea utake usitake.

Kila kitu kukiwaza hakiwezekani ndiyo hakitawezekana sababu muumbaji ni wewe.
Ukiwaza kama ni ngumu kuwa tajiri, njia rahisi za kutajirika utaziona haziwezekani.
Ndiyo maana ya kila kitu kinachokutokea maishani, kinatokana na wewe.

Turudi katika maandiko.
Sala yoyote unayoisali ni kuwa unazijaza hisia zako kujisikiliza mwenyewe.
Hivyo kuhisi ujasikilizwa ni kuwa hisia zako hazijapokea maagizo yako kwa uzito.
Ukihisi umesikilizwa ni kuwa hisia zako zimepokea maagizo yako kwa uzito hivyo utaona kidhahiri maombi yako yanatokea.
Yanatokea sababu wewe ndiye muumbaji na sehemu unayoanzia uumbaji Wako ni katika mawazo.

Kama uamini fanya utafiti.
Ukiona kitu ambacho hujawahi kukiona kabla, wazia sana kukiona tena.
Nakuhakikishia utaanza kukiona kila wakati.
Sawa na ukinunua kitu ambacho hujawahi kukiona mtaani, ukiingia mtaani utagundua watu wengi wanacho.

Katika sala ni hivyo pia, kadri unavyoamini ndivyo unavyofanikiwa.

Sala si lazima iwe tu kama kumwambia Mungu wa Mbinguni.
Hata maneno na mawazo yoyote unayojiwazia kwa kina yatatokea sababu wewe ndiye muumbaji.

Katika mafanikio ya jambo lolote, iwe dini, saikolojia, unashauriwa kujisemea kwa uzuri mala kwa mala, kujisemea kwa kufanikiwa mala kwa mala.

Kidini tendo hilo linaitwa imani, wakati kisaikolojia ni kuziimalisha fikra zako ili zitokee kidhahiri.

Marufuku, kujiwazia kila wakati, kama mimi nitakufa maskini, mimi sifanikiwi, mimi nitakufa mdogo, mimi ninaumwa sana, mimi ni mnyonge, mimi sipendwi, mimi sina akili, mimi nitafeli mtihani, sipati kazi n.k.

Ukiruhusu hizo fikra kujaa akilini, utayaona yanatokea live.
Na utamlaumu Mungu aliyejaza tayari kila kitu ndani yako.

Tuwe pamoja.
Sisi ni Afrika tu Umoja.
 
Back
Top Bottom