Nguvu za ushindani katika biashara (Competitive Forces Model)

Joined
Jul 3, 2016
Posts
19
Reaction score
13
Habari zenu wadau.
Ni matumaini yetu kwamba nyote mu wazima wa afya.

Kwa mara nyingine tena tungelipenda ku-share nanyi juu ya kile kiitwacho Nguvu za Kiushindani Katika Biashara (Competitive Forces Model).

Kwanza kabla ya yote ni vyema ndugu msomaji ukafahamu maana ya neno INDUSTRY, hichi ni kikundi au mjumuiko wa makampuni yanayotoa huduma au kuzalisha bidhaa zenye kukidhi mahitaji ya aina moja kwa mteja (Basic customer's needs). Kwa mfano carbonated drinks/soft drinks (Hivi ni vinywaji vitokanavyo na gesi ya carbon dioxide kuongezwa katika maji kwa njia ya mvuke na kuyachanganya na syrup), maji ya chupa (bottled water) na juisi zitokanazo na matunda (fruit punches). Bidhaa zote hizi hushabihiana (substitutes) na hukidhi hitaji moja kwa mteja ambalo ni kukata kiu. Hivyo kampuni zote zinazojihusisha na uzalishaji wa bidhaa hizi kama Coca-Cola, Cadbury Schweppres na PepsiCo zipo katika INDUSTRY moja ya utengenezaji wa vinywaji baridi.

Baada ya kuwa tumefahamu maana ya neno "Industry", sasa ni vyema tukazifahamu nguvu za ushindani katika "Industry" yoyote ile. Nguvu hizi (forces) zipo 5 ambazo ni:
  1. Madhara yatokanayo na kuingia mshindani mpya (risk of entry by potential competitor)
  2. Kiwango cha ushindani miongoni mwa wa washindani katika 'Industry" (Intensity of rivalry among established companies within industry)
  3. Nguvu ya mteja katika kushawishi bei ya bidhaa/huduma (Customer's bargaining power)
  4. Nguvu ya muuzaji katika kushawishi bei ya bidhaa/huduma (Supplier's bargaining power)
  5. Kiwango cha ushabihano wa bidhaa (Closeness of substitute to an industry)
Pindi hizi nguvu (forces) zinapokuwa thabiti (strong) huweza kukwamisha kampuni husika kupandisha bei ya bidhaa zake ili kupata faida kubwa. Kwa muktadha huu, pindi nguvu hizi (forces) zinapokuwa na uthabiti basi hutazamwa kama changamoto katika biashara (challenges/threats to competitive advantage). Hivyo ni wajibu wa mfanyabiashara kusuka mkakati (Business Strategy) ili kuzipunguza nguvu au uthabiti na hatimaye kufanya vyema katika "industry'.

Kwa upande mwingine, pindi hizi nguvu (forces) zinapokosa uthabiti (weak), basi huweza kutazamwa kama fursa (opportunities to competitive advantage). Hivyo inamuwajibikia mfanyabiashara kusuka mkakati (Business Strategy) ili aweze kufaidika na hali hii na hatimaye kuwa kinara katika 'industry"

Ahsanteni

Kwa huduma za:
  • Ushauri wa kitaalamu katika Business Development & Management,Project Management na Strategic Management.
  • Uandishi wa michanganuo ya biashara na miradi (Business Plans & Project Proposals).
  • Utoaji wa semina katika maeneo tutoleayo ushauri wa kitaalamu.
Usisite kututafuta kupitia 0719 518 367, 0783 695 639 au platinumconsultancy74@gmail.com
 
Hongera Sana mkuu kwa unavyotiririka, endelea kutupatia elimu hii ya ujasi na pia ntafika ofisin kwako soon.
 
Hongera Sana mkuu kwa unavyotiririka, endelea kutupatia elimu hii ya ujasi na pia ntafika ofisin kwako soon.
 


!
!
mwisho kabisa ungemtaja Prof Harry Porter kuwa ndio aliyeleta hiyo kitu ili mtu akagugo aongeze maarifa zaidi ya hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…