NHC Wanachemsha Katika Mradi wa Ujenzi wa Nyumba!

K-Boko

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Posts
697
Reaction score
218
NHC wana mradi mzuri wa ujenzi wa nyumba. Hivi kwanini wasingejenga ghorofa (condominiums) badala ya nyumba za kawaida (za chini) ambazo zinakula maeneo ya ardhi kuliko ghorofa ambaz0 ujenzi wake unahifadhi ardhi kwa sababu zinakwenda juu lakini zinachukua wakazi wengi? Pia ghorofa zinaleta shepu nzuri ya maeneo ya makazi vilevile.
 
Tatizo sisi waswahili huwa hatuna hob ya magorofa na tukizipata ni muda mfupi tuna piga bei na kwenda kibondi maji
 
mimi wanachoniudhi ni kuwa nyumba zao hazilengi mtanzania wa kawaida. sasa kama nyumba inauzwa mil 500 ni mtanzania yupi anayeweza kununua nyumba hiyo kama sio haohao mafisadi na matajiri waliopata hela zao kihalali wachache?
 
Wana shina na site planner wao, hayuko innovative wala modern, yuko more on plot badala ya all anemities za makazi
 
Tell me how u can build low cost house ya ghorofa???
sio mbaya pia tukaiandika lugha ya watu vizuri, ni '''''how u can........? au how can u..........?''''''' wataalamu wa ngeli turekebisheni hapa.
 
Tell me how u can build low cost house ya ghorofa???

"Low cost" ni shepu (structure) ya kitu au thamani ya kitu? Nina mfano hai pale Addis, Ethiopia, wanajenga nyumba za ghorofa hizo hizo "low cost"--nimeingia ndani na kuziona--nimetembelea nyingi tu pale mjini!
 
Tatizo sisi waswahili huwa hatuna hob ya magorofa na tukizipata ni muda mfupi tuna piga bei na kwenda kibondi maji

Sina hakika coz sijafika huko Michenzani, Zanzibar, lakini pia nasikia hizo ghorofa (za Karume) wanakaa watu wa kawaida tu. Sasa mzee kama kipato chako ni kidogo na umepata kisehemu chako cha vyumba viwili, sebule, choo na jiko, kwanini uuze kwenda Kibonde Maji?
 
mimi wanachoniudhi ni kuwa nyumba zao hazilengi mtanzania wa kawaida. sasa kama nyumba inauzwa mil 500 ni mtanzania yupi anayeweza kununua nyumba hiyo kama sio haohao mafisadi na matajiri waliopata hela zao kihalali wachache?

Ndio maana wanajenga nyumba za aina nyingi kulingana na mahitaji.
 
Sina hakika coz sijafika huko Michenzani, Zanzibar, lakini pia nasikia hizo ghorofa (za Karume) wanakaa watu wa kawaida tu. Sasa mzee kama kipato chako ni kidogo na umepata kisehemu chako cha vyumba viwili, sebule, choo na jiko, kwanini uuze kwenda Kibonde Maji?

Michenzani pale kupanga ni Laki2 kwa mwezi!!

Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana wanajenga nyumba za aina nyingi kulingana na mahitaji.
mkuu niambie nyumba za bei ya chini kabisa unazozifahamu zilizojengwa/zinazojengwa na NHC ambazo hata mwalimu anaweza kuzi-afford.
 
Tell me how u can build low cost house ya ghorofa???

Inawezekana. mbona Ethiopia wameweza. Tatizo serekali wanaona ujenzi wa nyumba kama njia ya watu kutajirika na ndio maana viwanja vinakuwa bei mbaya wakati wenye maeneo yaliyopimwa viwanja wanalipwa kiduchu.
 
NHC wana mradi mzuri wa ujenzi wa nyumba. Hivi kwanini wasingejenga ghorofa (condominiums) badala ya nyumba za kawaida (za chini) ambazo zinakula maeneo ya ardhi kuliko ghorofa ambaz0 ujenzi wake unahifadhi ardhi kwa sababu zinakwenda juu lakini zinachukua wakazi wengi? Pia ghorofa zinaleta shepu nzuri ya maeneo ya makazi vilevile.

Huku arusha wanajenga maghorofa ni wapi huko wanajenga hivyo?
 
Back
Top Bottom