NHC yaagizwa kuweka lengo la kutoa gawio la Tsh. Bilioni 10 kwa Serikali

NHC yaagizwa kuweka lengo la kutoa gawio la Tsh. Bilioni 10 kwa Serikali

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuweka lengo la kutoa gawio Serikalini la Tsh. Bilioni 10 kwa mwaka Ujao wa fedha.

Kauli hiyo ameitoa katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa NHC kilichofanyika mkoani Pwani mapema, Februari 24, 2025.

Akizungumza katika kikao hicho, Mchechu awakumbusha wafanyakazi wa NHC kuwa umoja, upendo, na mshikamano katika utendaji wao wa kazi ni muhimu kwa maendeleo ya taasisi hiyo.

Amesema kuwa, bila kushirikiana, taasisi hiyo itakuwa ngumu kufikia malengo yake ya kiuchumi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Ahmad Abdallah, amewakumbusha wafanyakazi kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa uwadilifu na katika muda uliotakiwa.
IMG-20250224-WA0179.jpg

IMG-20250224-WA0137.jpg

IMG-20250224-WA0163.jpg

Chanzo: Torchmedia
 
Back
Top Bottom