DOKEZO NHIF hawajatulipa Watoa Huduma kwa miezi mitano, wanatupa ugumu kuhudumia wenye uhitaji

DOKEZO NHIF hawajatulipa Watoa Huduma kwa miezi mitano, wanatupa ugumu kuhudumia wenye uhitaji

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mmoja wa watu ambao nimekuwa nikifanya kazi kwa ukaribu na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), sina nafasi hiyo ya juu lakini nipo katika sehemu ambayo NHIF wakitimiza wajibu wao itakuwa ni furaha kwangu.

Lakini ninachokiona ni kuwa Mfuko huo ni kama umepoteza uwezo wa kulipa fedha kwa watoa huduma wake, kwa sasa watoa huduma wengi hawajalipwa madai ya zaidi ya Miezi 5, kutokulipwa kwao kunasababisha pia sisi wengine tuwe na maisha magumu.

Wengi wetu hatujalipwa mishahara na malipo mengine kwa kuwa waajiri wetu wanategemea kulipwa na NHIF ili nao waweze kutulipa, hivyo huo mnyororo unaathiri sana maisha yetu,

Najua Mkataba unawataka NHIF kulipa watoa huduma ndani ya siku 60 tangu walipowasilisha madai, kwa sasa hali ni tofauti kwa watoa huduma kwani wapo wanaodai fedha walizohudumia wanachama wa NHIF tangu mwezi wa 6 Mwaka huu 2023 ambao ni muda wa miezi 5, hiyo ni kinyume na mkataba.

Malipo in 60 Days.jpg


Tumekuwa tukijaribu kuulizia sababu za wao kuchelewesha malipo kwa muda wote huo, sababu wanazotoa ni kuwa hawajapokea fedha kutoka Hazina kwa kuwa wameishiwa fedha.

Kitendo hiki kinavunja mkataba na kuathiri ubora wa utoaji huduma za afya nchini hasa tunapoelekea Afya kwa wote.

Nashauri NHIF ilipe madai yetu sisi watoa huduma kwa mujibu wa mkataba.

====

Pia soma: Hospitali za private (binafsi) zatishia kutohudumia wagonjwa wanaotumia bima ya afya ya NHIF
 
Halafu pesa za kuendesha huo mfuko ikiwemo kuwalipa watumishi wake haziwezi kukosekana abadani.

Service Providers endeleeni kumuomba Mungu
 
Hii NHIF mimi binafsi naiona ni upuuzi puuzi tu, nimemkatia bima ya ofisini mtoto wangu ila kila kipindi atakachoumwa dawa ni lazima ni gharamikie. Si bora tu nimkatie bima zenye wanajitambua??!!. Ukija huku mitandaoni unakuta hawalipi watoa huduma, upuuzi mtupu
 
Btw naangalia utaratibu wa kutolewa kwenye kuchangia bima ya afya inayotolewa na NHIF, bora nichangie bima kwengine kwenye uhakika wa huduma
 
Na watu kukatwa kila mwezi ni kama kawa..kinachofanya washindwe kilipa watoa huduma ni nini??

Hii nchi ifike mahali tuonyeshe kuwa tupo serious hata kwa kuingia msituni..
 
Back
Top Bottom