NHIF hili ni tatizo la kiufundi, mnaibiwa au mnajiibia?

NHIF hili ni tatizo la kiufundi, mnaibiwa au mnajiibia?

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
Inakuwaje napokea taarifa za kutumika kwa kadi yangu ya bima ya afya wakati sijaenda hospital na kadi ninayo?

Tarehe 11 mwezi huu nimeenda hospital X nimepatiwa huduma na nimepata notification msg kuwa kadi yangu imetumika katika hospitali hiyo, nimechukua kadi yangu nimeondoka nayo.

Leo tarehe 13 natumiwa msg nyingine kuwa kadi imetumika saa 3 asubuhi katka hospitali hiyohiyo wakati nipo nyumbani nimetulia sijaenda popote, hii inaitwaje kitaalamu?

Naombeni ufafanuzi maana nawapigia kutoa taarifa ya kutotambua huo muamala hampokei simu, wasije wakanibambika magonjwa ya ajabu mimi huko!
 
Wakati nina bima yao enzi zile za kichuo, iliwahi kunitokea hiyo.

Nahisi ni hosp wanacheat ionekane wametibia mara nyingi kumbe ni wana duplicate, ama sivyo basi ni tatizo la system.
 
NHIF imeshageuzwa shamba la miwa la bibi
 
Mwisho wa dunia sijui unasubilia nn,mambo ya hovyo kweli,tanesco na zimamoto angalau wanapokeaga
 
Siku hiyo uliyoenda hospitali ulipata message?
 
Siku hiyo uliyoenda hospitali ulipata message?
Nilipata message siku hiyohiyo,nashangaa leo tena wananitumia message tena yenye ref# tofauti na ile ya siku ile inaonekana ni muamala mpya kabisa
 
waripoti, hiyo ni fraud na ndio wanasabisha mfuko unaelemewa na matumizi kuliko mapato,wanatibiwa watu hewa au wasio wachangiaji kwa hela yako,mwisho wa siku mfuko unaelemewa na ndio inapelekea kupunguzwa huduma za vifurushi
 
Pole mkuu!

Ukiangalia hizo sms mbili utagundua kuna tofauti.

Ya kwanza, inakupa taarifa kuwa card yako imetika hospital xx

Ya pili inakupa taarifa ya gharama ambazo umetumia kwenye hiyo hospital xx

Nb: mimi sio mfanyakazi wa NHIF, nimejibu kutokana na uzoefu nilio nao!
 
Ni sehemu nzuri sana ya kujipigia hela maana hakuna usimamizi imara wa hizi Bima
 
NHIF Huwa wanapgwa San especially Kwa hizi hospital au dispensary za private unakuta unatibiwa malaria vipimo na dawa tu unakuta wanakuletea sms umetumia elfu 75, aise mpka nilishtuka.
 
NHIF Huwa wanapgwa San especially Kwa hizi hospital au dispensary za private unakuta unatibiwa malaria vipimo na dawa tu unakuta wanakuletea sms umetumia elfu 75, aise mpka nilishtuka.
Mkuu kuna kitu naona watu hamkielewi.
Bei za huduma na dawa ambazo zinatuka kwenye kila hospital ni makubaliano baina ya hospital na NHIF au Bima yoyote ya afya.

Mtoa huduma hawezi kutumia bei ambazo hajakubaliana na Bima ya Afya.

Kwa hiyo NHIF hawapigwi, bali wanajipiga wenyewe kwa kuingia mikataba ya kupewa huduma kwa gharama kubwa.
 
Pole mkuu!

Ukiangalia hizo sms mbili utagundua kuna tofauti.

Ya kwanza, inakupa taarifa kuwa card yako imetika hospital xx

Ya pili inakupa taarifa ya gharama ambazo umetumia kwenye hiyo hospital xx

Nb: mimi sio mfanyakazi wa NHIF, nimejibu kutokana na uzoefu nilio nao!
Sio hivi ulivyozungumza wewe,nimeletewa msg za kutumika kwa kadi ma sio gharama za huduma
 
Sio hivi ulivyozungumza wewe,nimeletewa msg za kutumika kwa kadi ma sio gharama za huduma
Ooh.. Pole sana..
Lakini pia kama umeonana na specialists wawili tofauti, pia inaweza ikawa sababu.

Kwa huduma zaidi, wapigie simu NHIF watakupa majibu mujarabu kabisa!
 
Inakuwaje napokea taarifa za kutumika kwa kadi yangu ya bima ya afya wakati sijaenda hospital na kadi ninayo?

Tarehe 11 mwezi huu nimeenda hospital X nimepatiwa huduma na nimepata notification msg kuwa kadi yangu imetumika katika hospitali hiyo, nimechukua kadi yangu nimeondoka nayo.

Leo tarehe 13 natumiwa msg nyingine kuwa kadi imetumika saa 3 asubuhi katka hospitali hiyohiyo wakati nipo nyumbani nimetulia sijaenda popote, hii inaitwaje kitaalamu?

Naombeni ufafanuzi maana nawapigia kutoa taarifa ya kutotambua huo muamala hampokei simu, wasije wakanibambika magonjwa ya ajabu mimi huko!
Fraud hiyo, huo mchezo unafanyika Sana kwenye private hospitals hasa dispensaries Na polyclinics.

Tatizo ni kwamba hata hao NHIF wenyewe nahisi wanaujua huu mchezo Ila ndio hivyo Shamba la Bibi kila mtu mvunaji.
 
Back
Top Bottom