Blasio Kachuchu
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 366
- 243
Habari NHIF,
Mimi naomba kutoa malalaniko yangu kwa hizi shule za msingi ambazo mlipeleka uratibu wa Bima Shuleni (Afya Toto Card)... tuchukulie mashuleni. Ila kinachonisikitisha ni jinsi hizi shule zimeona hilo ni dili na kujipangia bei badala ile elekezi ya 50,400 wao wameweka 65,000/= wanawachaji wazazi. Nina mifano halisi ya shule kadhaa kama Fountain Of Joy Pre&Primary School ya Mbezi Mwisho wao wanataka wazazi walipe 65,000/= jambo ambalo si sawa. Jiulize 14,600/= inakwenda wapi??
Jifikirie kwa watoto 100 wanavuna hela ngapi? Huu ni utapeli kwa wawazi kabisa. Hili suala wahusika NHIF kama mmeshindwa utaribu wa hili jambo angalieni namna ya kusolve tatizo, watu wanajivunia hela kupitia nyingi.
Waziri Jenista wapange watu wako huku wazazi tunaibiwa.