NHIF mjue kwamba jinsi nchi inavyoendelea ndivyo magonjwa ya kuambukiza yanavyopungua na yale yasiyoyakuambukiza kuonekana zaidi

NHIF mjue kwamba jinsi nchi inavyoendelea ndivyo magonjwa ya kuambukiza yanavyopungua na yale yasiyoyakuambukiza kuonekana zaidi

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,119
Reaction score
4,569
Inashangaza kusikia NHIF ikilalamika kuwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCDs) yameongezeka sana, gharama ya matibabu yake ni kubwa sana na yanafilisi mfuko. Na kwamba NHIF inakusudia kuacha kugharimia matibabu ya magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza.

Kama tetesi hizi ni za kweli, basi hakuna sababu ya kuwepo mfuko huo bima ya matibabu. Magonjwa ya kuambukiza ni kama malaria, minyoo, typhoid, kipindupindu, kaswende, kisonono na kichocho. Gharama ya matibabu yake ni ndogo sana na mtu hahitaji kuwa na bima ya matibabu yake.

Magonjwa yasiyo kuwa ya kuambukiza ni kama yale ya saratani, kisukari, shinikizo la damu, Figo na moyo. Gharama ya matibabu yake ni kubwa na hivyo ndiyo yanayohitaji bima. Maana ya bima ni hiyo. Mtu hakati bima kwa matatizo madogo madogo kama ya minyoo au kisonono.

Jinsi nchi yetu na watu wake wanavyoendelea kiuchumi, magonjwa ya kuambukiza yanaendelea kupungua na mengine mengi kuwa historia. Usambazaji wa maji safi na salama kwa kila mtanzania utatokomeza magonjwa kama ya typhoid, dysentery, amoeba etc. Makazi bora yatatokomeza magonjwa kama ya malaria, pneumonia, homa ya uti wa mgongo etc. Uvaaji wa viatu utatokomeza magonjwa ya minyoo. Utumiaji wa Ngorongoro salaama utatokomeza magonjwa ya zinaa kama yale ya kaswende, kisonono, UTI na HIV. Lishe bora itatokomeza magonjwa mengi sana yakiwemo ya kuambukiza na yasiyokuwa ya kuambukiza.

Hayo ndiyo matokeo ya maendeleo ambayo bima ya afya ya taifa inapaswa kujipanga. Serikali pia inabidi kuhamasisha bima za afya za watu au makampuni binafsi kuanzishwa kwa ajili ya wale wenye uwezo ili kutoa ushindani.
 
Back
Top Bottom