Singo Batan
JF-Expert Member
- Apr 24, 2020
- 295
- 198
Mwanzoni wakati mfuko huu unaanzishwa ulikuwa unafanya vizuri sana kwasababu ulikuwa unachangiwa na Watumishi wa umma na kuwahudumia watumishi wa umma. Mfuko ulikuwa stable sana. Tatizo lilianza mlipoingiza tamaa za kuufanya kuwa mfuko wa biashara badala ya huduma.
Haikupaswa taha kidogo kuufanya mfuku huu uhudumie kundi kubwa la watu kabla hamjafanya utafiti wa kutosha kama mnaweza kuwahudumia. Watumishi na wategemezi wa watumishi waliwatosha sana kuwahudumia. Mlichotakiwa kufanya ni kutoa mapendekezo ya kuanzishwa kwa bima ya wananchi wote nje ya watumishi, na mfuko wenu ungekuwa unachangia shirika hilo jipya linalohudumia wananchi wote ambao sio wanufaika wa NHIF.
Madhara ya kujitanua bila utafiti wa kutosha kuhusu gharama za uendeshaji wa shirika ni haya yanayojitokeza sasa, kupunguza huduma na kushindwa kukidhi matarajio ya wateja wenu hasa wale mlioanza nao. Ushauri kwenu kaeni na CHF boresheni models za huduma huko na ifanyeni ikidhi standards za kitaifa kamailivyo NHIF kisha mpunguze idadi kubwa ya wateja wanaoelekea kuwashinda na kuufilisi mfuko wenu.
jikiteni kwenye huduma ya msingi ili msiharibikiwe zaidi. wateja hawategemei kushushiwa au kupunguziwa viwango vya huduma badala yake viwango vinapaswa kuongezeka. Zile ni fedha zao sio hisani mnatoa