DidYouKnow
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 1,229
- 1,950
Nimempeleka bimkubwa katika mojawapo ya hospitali ya serikali hapa jijini Dar.
Ana shida ya mgongo, vidonda vya tumbo, na presha. Leo alipaswa aonwe na madaktari watatu, daktari wa moyo, mifupa na utumbo.
Kwa sababu hospitali hii ina daktari bingwa wa mifupa na daktari bobezi wa moyo, nilitegemea tukionwa na daktari wa mifupa, tutaruhusiwa kuonwa na mbobezi wa moyo.
Ajabu tulipotoka kwa daktari bingwa wa mifupa, tumezuiwa kumwona daktari mbobezi wa moyo, ati kuanzia sasa ukitoka kwa daktari bingwa idara moja huruhusiwi kuonwa na daktari mbobezi wa idara nyingine isipokuwa huyo daktari naye awe level moja na yule aliyekuona mwanzo, na vice versa is true.
Wametuambia kama tunamtaka sana daktari wa moyo basi tuje siku ya pili. Sijaelewa hii mantiki.
Mbona NHIF mnafanya maisha kuwa magumu sana?