NHIF na Toto Afya kadi mashuleni hakuna msukomo wa usajili

NHIF na Toto Afya kadi mashuleni hakuna msukomo wa usajili

Mwanga Mkali

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2018
Posts
1,302
Reaction score
2,473
Salaam,

Mh. Ummy Mwalimu mwaka 2017 pale mnazi mmoja alizindua Toto Afya kadi kwa lengo la kusajili watoto 10m kati ya 25m walio kuwepo wakati huo ili kunusuru afya za watoto wetu kabla ya maradhi. Kampeni hii ili ishia kushindwa kwa kusajili watoto +240k ambao michango yao ilikuwa si zaidi ya 5bilioni na matumizi yao yalifika 40bilioni hivyo lengo la kusajili watoto wengi kutotimia na matumizi ya kuwahudumia kuwa tishio la afya ya mfuko. Hii imepelekea mfuko kusitisha usajili huu kwa watoto binafsi na kuwalazimisha wazazi wasio waajiriwa au wenye wategemezi kuwaunganisha watoto kwenye vifurishi vipya.

Nini imekuwa sababu ya kushindwa huku kufikia lengo la watoto 10m? Sababu kuu zimegawanyika kwenye maeneo matatu moja ni umasikini mbili uhamasishaji mdogo kwa wadau na tatu uelewa wa jamii kuhusu mfuko.

Leo ntajikita kwenye uhamasishaji mdogo na uelewa, hii ni baada ya mapitio kuja na utaratibu mpya wa usajili kwa watoto chini ya miaka 18. Ambapo kwa sasa ni mpaka miaka 24 kwa wanavyuo.

Toka utaratibu huu uanze NHIF haijafanya uhamasishaji wa kutosha kwenye shule za msingi nchini kote kuhamasisha kujisajili kama wakala wa NHIF ili watoto wengi wasio na kadi kujiandikisha. Badala yake wazazi wasio waajiriwa au wenye wategemezi wenye uwezo wa kulipia 50400 kushindwa kuwasajili watoto wao kwenye mfuko.

Shule za serikali zinazopokea wanafunzi wa kidato cha tano na vyuo vya kati nao ni changamoto kwa kuwa mpaka sasa wamepokea michango hiyo na watoto kwa idadi kubwa hawajapatiwa kadi. HUU NI WIZI PIA.

Nawashauri NHIF kuhimiza usajili wa shule za msingi kuwa takwa la lazima ikiwezekana waombe Bunge kuwapitishia sheria ili wazazi wote wawasajili watoto. Bila hivyo kampeni hii itakufa kabisa kama inavyokufa sasa.
 
Mazingira ya ushawishi yamekaa kirushwa na kisiri ili kuendeleza upigaji wa afya kwenye huduma.
 
Back
Top Bottom