DOKEZO NHIF ofisi ya Bandari boresheni huduma

DOKEZO NHIF ofisi ya Bandari boresheni huduma

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

willpower

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2019
Posts
408
Reaction score
2,314
Wadau,

Mara kadhaa kwa sababu za kijiografia imekuwa ikinilazimu kupata huduma za NHIF katika ofisi zile zilizo bandarini, kwa kweli huduma za pale mapokezi ambao pia ndio wanaopokea fomu na kuwasikiliza wateja wahusika wa hili tawi la NHIF watupie macho hapo kwenye hicho kitengo.

Matatizo ya mapokezi ni kama ifuatavyo;

1. Hawana mpangilio wa kazi kabisa, wapo maafisa wanne (4) lakini hawana mgawanyo wa kazi. Yaani kati yao wanafanya kazi zinazofanana.

2. Hawajali kuhusu muda kabisa, yaani wao ni stori zao badala ya kazi. Kama unasubiri lipa namba ili ufanye malipo unaweza kutumia masaa matatu kusubiri hiyo namba.

Wenye hii ofisi badilikeni, kazi za umma hazifanywi hivyo.
 
Back
Top Bottom