Ni aibu Graduate wengi kumaliza chuo hawezi kujitegemea. Nashauri wasipewe vyeti hadi kuwe na ushahidi wa kujitegemea

Naunga mkono hoja hiyo ndio iwe kigezo Cha kupewa cheti yaani field
 
We kuweza?
 
Kuna member wakipost uzi ukisoma heading unasema yes asikilizwe anakitu lakini ukiusoma uzi wenyewe unakuja kugundua huyo member ni zero brain kabisa mfano huu uzi.
Ntauboresha kwa kuupa point zenye mashiko ili hao graduate wapate challenge kwa kujua shida iko wapi lakini nianze na mtoa mada.
Unavyosema la saba /form four anaendesha maisha yake kwa :-
•kuchoma mahindi •kunyoa •umama / ubaba ntilie kwanini graduates wasiendeshe maisha yao kwa hizo kazi swali ni je mliwasomesha ili waje wafanye hizo kazi? If not kwanini uteme nyongo kwenye kitu ambacho hata wewe hukijui or ndo kusema ukijipata kidogo tu basi wengine wote wanazingua unafumbia macho factors kama Muda, mfumo wa elimu na system yote ya nchi ambayo imeshindwa kuwaaccomodate or kuwajengea uwezo hao wasomi.

By then heading ya uzi ni nzuri sana so tatizo liko wapi why graduates hawana udhubutu why hawawezi kufikiria outside the box?

Jibu lipo kwenye utafiti wa tabia uliofanyika kwa nzi ambapo tabia hizo zinafanana na tabia za binadamu.
Kilichofanyika ni walichukuliwa nzi wakafungiwa kwenye jar for 3 days then after 3 days jar ikafunguliwa what happened ni hao nzi hawakuweza tena kupaa zaidi ya urefu wa hiyo jar maisha yao yote (nimeambatanisha video)
Like wise kwa mfumo wetu wa elimu ambao mimi naufananisha na hiyo Jar ambapo unamchukua mtoto akiwa mdogo 5-6 years wanakurudishia ana 22 years and above kule hajifunzi skills zozote zaidi ya kile anachosomea tu, mbaya zaidi mfumo uko programed mtu asome ili aje kuajiriwa in that case what do you expect.
Your browser is not able to display this video.
 
Hizo kazi zote wanaozifanya ni graduates. Issue ni mfumo wa elimu, nakumbuka kipindi tunaanza la darasa la kwanza 1995 walimu walituuliza mnasoma ili mfanye kazi gani wengi wetu tulisema ualimu, udaktari, urubani n.k Elimu iliandaa wanafunzi wasome ili waajiriwe. Kaka usilaumu kwa vile upo hapo ulipo kwa connection ya shemeji yako aliyemuoa dada yako.
 
Tatizo mtaji mkuu hakuna anependa kukaa home akiwa 28+, Pia elimu yetu inatengeneza wahitimu wakuajiriwa kuliko wakujiajiri.
 
Labda tujaribu biashara ya ku export mkaa kutoka Tanzania kwenda Ulaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…