Ni aibu kubwa kwa wana Arusha kuwekewa kiingilio kama hiki

Hivi Kiingilio huwa kinapangwa kwa kuzingatia hali ya Uchumi wa eneo husika na Watu husika kwa Kipindi husika au huwa kinapangwa kwa kuzingatia aibu?
Mimi sijui wanaangalia nini.....
 
wewe ulitaka wawekewe kingilio shingapi...
 
Mimi sijui wanaangalia nini.....

Nadhani kama hujui huwa wanaangalia nini basi hukupashwa kusema kuwa ni ' aibu ' kwa wana Arusha. Halafu wala haiitaji akili kubwa sana kutaka kujua ni kwanini TFF imeweka Kiingilio kidogo kama hicho katika hiyo Fainali ya ASFC. Kumbuka Mkoa wa Arusha kwa muda mrefu sasa hauna Timu yoyote VPL hivyo wakazi wa Arusha ni kama vile mwamko wao katika Kupenda mchezo wa Soka umeshuka kama siyo kupungua sana na njia pekee ya kurudisha ' hamasa ' na ' kuwavutia ' Watu warudishe mapenzi yao katika mchezo Kwanza ni kuwapelekea mechi muhimu kama ile halafu unawakea Kiingilio kidogo sawa na bure ili kuwatia moyo kisha na Wao sasa wajitahidi kuzipigania Timu zao ili basi ziweze kufanya vyema katika Ligi mbalimbali na zipande Ligi Kuu ya VPL na Mkoa uwe na Timu. Kama kuna Mkoa ambao ni dhambi sana kwa wenyewe kutokuwa na Timu VPL basi ni wa Arusha hasa kutokana na umuhimu wake ' strategically ' na ' economically '.

Kila la kheri.
 
aiseee hii ni ayubu(in panjuan voice) kwa mabillionaire wa Arusha aiseee
 
Arusha wawekee mkutano wa CDM watatoa hata hela kuhudhuria...ila habari ya Mtibwa na Singida Utd utashangaa hata hiyo 1,000 watu hawatatoa.
 

Sio kupenda soka ni kupenda soka la nchini, watu tunafatilia ligi za nje zaidi ya za ndani. Hiko kiingilio ni kuvutia watu zaidi hasa vijana wenye umri mdogo.
Usitarajie umpate mzee au baba wa kwenda kuangalia mechi kama hiyo.
 
Arusha wawekee mkutano wa CDM watatoa hata hela kuhudhuria...ila habari ya Mtibwa na Singida Utd utashangaa hata hiyo 1,000 watu hawatatoa.
Basi wangefanya bure kabisa na suala ni kuhamasisha soka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…