Ni aibu kwa CCM kujipeleka Zambia bila kualikwa

Upinzani ni pale unapokuwa NJE YA MADARAKA.....ukishayapata tu wewe ni CHAMA TAWALA na si mpinzani tena.....

Makada wa CCM kuwepo huko ni sahihi.....

Mh.Hichilema ni rais mpya wa Zambia(man in show).....sasa tuone ATATHUBUTU KUTOKURUDI KUWA MPINZANI AMA NDIO IMEANZA SAFARI YA MUDA MREFU YA CHAMA CHAKE ndani ya muungano wao?!!!!


#KaziIendelee
#NchiKwanza
#SiempreCCM
 
Ccm wamekwenda kuzamia shughuli ya watu kama kawaida yao hakuna watakachofanya cha zaidi ya kuonekana tu kama kwaya fulani kutoka tanzania iliyokosa nafasi ya kutumbuiza kwenye sherehe.
 
Kwanza siyo kweli kwamba SSH na URT hatukualikwa kwenye sherehe hizi. Huu ni UONGO
ULIOKITHITRI! Kama hatukualikwa, hata hilo dege letu lisingepewa kibali cha kuingia Zambia, huo ndio utaratibu wa kimataifa. Uongo kama huu haufai humu JF. Hata hilo gwaride la kupokelewa SSH lisinge fanyika; huu ni uongo kama wa akina TOBO!

Halafu hizo quotations hapo juu ni kutoka kwenye vyombo na vyanzo gani? Hukuviweka bayana hivyo huo nao ni uzushi wa kawaida tu kwenye dunia hii ya sayansi na teknolojia. Hata hivyo sisi tunajua hao ni akina nani na nia yao ni nini! Tujaribu kuwa wa kweli ili tupate elimu humu JF jamani!
 
Usipoalikwa utapokelewa na Nani? Utalala wapi? Kwenye sherehe utakaa wapi? Acheni akili za nyumbu hakuna kiongozi wa nchi anaweza kwenda nchi nyingine bila mwaliko.

Hawakualikwa wanaccm, kulitolewa nafasi kadhaa ndio wakaona wabebe wanaccm. Ccm wameona wivu ACT kualikwa, hivyo imebidi wajipeleke kwa lazima ili waseme wao ndio wako madarakani na sio ACT.
 

Nature ya mwanadamu Ni kushambulia pale alipopashindwa. Hawezi hangaika na kibudu kisicho na nguvu wala pumzi.

Ugonjwa wa kujifariji mnaounwa wanasiasa uchwara hautawaacha salama.
 
Wanatia aibu sana chama chakavu!
Mkuu kumbuka chama tawala hata kama kimetokana na upinzani, kikishinda tu tayari chama kilichoshindwa ndiyo chama cha upinzani. Kwa hiyo size ya akina Zitto ni Lungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…