Ni aibu kwa nchi za Afrika zinazoimba nyimbo za Taifa kwa lugha za kigeni

Ni aibu kwa nchi za Afrika zinazoimba nyimbo za Taifa kwa lugha za kigeni

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Zamani hata kabla ya kuja wageni na dini za kigeni waafrika walimwomba Mungu kwa lugha zao na kulikuwa na matokeo ya haraka sana kuliko sasa katika dini za kigeni.

Kuimba wimbo wa taifa kwa Kiingereza au Kireno au Kiarabu au Kifaransa hii ni sawa na kumkosea Mungu heshima, naipongeza Tanzania na Afrika ya kusini kwa kutumia lugha ambazo aliziweka Mungu katika ardhi hizo, hii inamaana ya kumsifu Mungu kwa kazi aliyoifanya ya kutupa lugha zetu yeye mwenyewe.

Kutumia lugha ya wimbo wa taifa la mtu aliye kuuza kama kuku ni kosa kubwa. Ata Mungu anashangaa.

Mtoto wa Mchungaji.
 
Ni sawa unavyo sema ila Sasa kwa nchi zenye lugha zaid ya moja wataimba aje?
 
Na kuimba kwa mseto wa lugha za "siwa hili" yaani "sahil" ni sawa?
 
Utandawazi ni kama mtego wa buibui. Utandawazi umebeba mengi wewe uwaye yeyote usijilazimishe kuyachukia mambo (cultural diversity) ya utandawazi.

Misingi yake imeanzia Roman Empire ikaendelea na uvumbuzi wa viwanda ulaya na maendeleo yake yakaibua haja ya Ukoloni.

Na ukoloni ulifanya yake na ukahakikisha utajipeleka mtegoni utandawazini (utanda buibui).
Adui usiyemuweza, hamia kwake au ufe tu.
 
Back
Top Bottom