Ni Aibu Kwa Tanzania Kuzidiwa na Uganda, Rwanda na Kenya Kuvutia Utalii wa Mikutano Wakati tuna Utajiri wa Vivutio vya Utalii

Zanzibar iko juu kwa ushoga labda wazungu wanakuja kuwafumua marinda
Ndio tatizo lenu maana hata kwenu wapo wakina Noel Mushi , yule aliyabdili jinsia , yule aliyoelewa pale kanisani Arusha ...
 
Utalii hamzidiani, kila sehemu kuna vitu tofauti, mtalii anachagua anachotaka kuangalia. Mfano mtalii hawezi kwenda Uganda kupanda mlima kilimanjaro, au aende Rwanda ili kuangalia mbuga ya Serengeti. Kila sehemu ina vivutio vyake hatushindani.
 
Karibu Arusha mkuu mji mzuri hali nzuri ya hewa .
Mgeni akija Tanzania bila kifika Arusha safari yake haijakamilika
Kwani nan amekuambia hajafika Arusha ? Tanzania yote DAR ndio kila kitu , huko siwezi kufika kwa vile sipatani na baridi nishazoea joto.
 
Kwani nan amekuambia hajafika Arusha ? Tanzania yote DAR ndio kila kitu , huko siwezi kufika kwa vile sipatani na baridi nishazoea joto.
Dunia nzima watu wenye akili wanakaa kwenye baridi
 
Wadudu ndio wanakaa kweny baridi , lakini hawavai mitumba hakuna mweny akili timamu anavaa mitumba
Wadudu wana stawi kwenye joto sio baridi. Mbona mnavaaa kanzu na makobazi waliyotupa waarabu
 
Mna vivitio lakini hamna hoteli kubwa za kulaza mikutano hii. Pia hamna ndege zenu zenye kubeba watu wengi. Mnakimbilia kuweka tozo kubwa kwenye vivutio badala ya kuangalia makusanyo ambayo mtapata kwenye kodi za hoteli na huduma nyengine, mnakomaa kwenye visa, airport tax, viongilio mbugani. Mfano, kuna nchi zina hoteli za vyumba 3,000 - 5000 so mkutano mmoja unatumia hoteli moja bila kuathiri huduma nyengine.
 
mi nadhani hata kuwemo kwenye hiyo kumi bora tumependelewa, sawa tunazo kumbi nzuri za kisasa na nyingine zinajengwa lakini kuna zaidi ya hilo, generosity ya watu wake hali ya hewa, usafi wa miji yetu, si mnakumbuka Michael jacton alikuja Dar akafikia Kilimanjalo Hotel akaondoka anasema Nchi inanuka shombo yote ya ufukowa bahari harufu ya samaki zinazochomwa magogoni kidogo vingenyofoa pua yake.
Nenda Kigali anzia tu air pot unajihisi pumziko furani na utulivu wa akili hawana kumbi nyingi wala zi nzuri kuliko zetu, hayo mengine ninayoyataja yanamfanya mshiriki ajihisi pumziko. kwetu sasa mtu anashuka airport kwanza ni joto lililochamana na harufu mbayambaya mtaani anapishana na marundo ya taka kama vile magari ya kuzoa taka hayakuwahi kununuliwa, mifuko ya plastick iliyokuwa imepotea awamu ya 5 imezagaa utafikiri Nchi haina mwenyewe wakati yupo, barabara zimejaa michanga utafikiri lami haikuwahi kujengwa na viongozi wapo. akitakaaende kaliakoo kwa sifa ya soko kubwa anaondoka huko ameugua kichwa hapa kuna spika hapa generator pale mpiga debe wakati sheria za kudhibiti sauti zipo lakini hazifuatwi hao maafisa mazingira wa ninisasa?
Rwanda mitaa inasafishwa na wanamtaa, imefikia hatua hata barabara zenye lami au mawe zinajenge na wenye mtaa wanachanga na serikali inafanya kwa yale ambayo wannchi hawawezi, sisi huku hata fedha inayotolewa na serikali viongozi wanakula. Eeee wanakula si waliambiwa wale kwa urefu wa kamba yao.
kwa ujumla bado tuko mbali sana ktk masuala ya kuithamini Nchi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…