Hoja hapa ni kuwa, kwanini wasomi wa elimu ya juu wamegeuka wasaliti na wapotoshaji wa kiwango cha juu kuhusu masuala nyeti hasa ya wizi wa fedha na rasilimali za umma kwa umma ili hali ukweli wanaujua? Ni nani sasa atasaidia kuuelimisha na kuuambia umma ukweli hasa wale waliokosa elimu?
Tumewashuhudia kina Dr. Bana & co wanavyojipa airtime kuupotosha ukweli. Ni nini maana ya wao kuitwa wasomi? Na sasa wanachuo nao wameamua kujiingiza kichwakichwa kuusaidia utawala wa mafisadi kuiba.
Hivi hawajajua kuwa ile benki ya standardchater ya hongkong kuna siku watakuja kuidai pesa yao baada ya kushinda kesi na tutakiwa kuilipa kama tulivyoilipa dowans. Tutafakri kwa usomi wetu jinsi ya kuiokoa nchi kutoka katika mikono ya mafisadi na sio kuungaunga mkono masuala yaliyowazi kabisa ambayo hata wale waliojiita wazee wa dar waliushtukia mchezo mchafu wa kulindana. Jifunzeni kuisoma lugha ya mwili (body language). Usomi wetu uwe na maana ya kujikomboa kifikra na siyo kujikomba kwa fikra za wengine.