Nasema ni aibu kwa wasomi wetu wa kada mbalimbali hapa nchini ambao wanategemewa na jamii kubwa ya watanzania katika kuleta mabadiliko na kuchochea maendeleo katika jamii watokazo,ni kama wiki moja sasa imepita tangu nilete uzi humu jamvini kuhusu kilichokuwa kinaendelea katka harakati za uchaguzi wa nafasi ya urais chuoni hapo na jinsi mizengwe mbalimbali ilivyokuwa inaendelea baada ya kila mgombea kubeba taswira ya uchama baina ya CDM na CCM chuoni hapo,bt me kama kijana msomi nimesikitishwa na kuumizwa baada ya kupokea taarifa ya jumla kamili ya wanachuo wa SAUT waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo ,ambapo kati ya wanafunzi 13500 waliopo chuoni hapo ni jumla ya wanafunzi elfu 3000 na....ndio waliojitokeza kupiga kura ya kuwachagua wabunge na kumchagua rais wa chuo hicho,ambapo Donavankamwene Mcheshi anaedaiwa kuwa kamanda wa CDM kumshinda mpinzani wake anaedaiwa pia kuwa kada wa CCM bwana Peter Bega katika uchaguzi uliofanyika jana chuoni hapo,kwakweli ni aibu kwa kuwa siku yote ya jana pindi uchaguzi unaendelea na vipindi vilikuwa vikiendelea madarasani bt wanafunzi walikuwa wanatoka darasani na kuvipita vituo vya kupigia kura na kuondoka bila kupiga kura,kwakweli hii ni changamoto kwa wasomi wa Tanzania,itakuwaje kama wataenda huko makwao,watawashauri nini ndugu zao,kaka ,dada na rafiki zao ambao si tu kwamba hawajaenda shule bali hata IQ yao ni ndogo na ya kawaida sana,itakuwaje hapo 2015?vijana na wasomi tuone umuhimu wa kushiriki katika michakato ya kidemokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa la sivyo tutabaki kulalamika kuwa tunaibiwa kura.