Ni aidha umpende mwanamke au umuelewe. Ila sio vyote.

Zemanda

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
8,323
Reaction score
18,051
Katika maisha yetu kama wanaume eneo la mahusiano na wanawake tunazo option mbili. Ya kwanza ni kumpenda mwanamke na ya pili ni kumuelewa mwanamke.

Katika hizi option mbili, huwezi zifanyia utekelezaji zote mbili kwa wakati m'moja. Lazima uchague moja nyingine uache iende.

Ukichagua kupenda mwanamke then usihangaike kumuelewa sababu itakupa ukichaa na hautakuwa na amani na kila siku utaamka na theories, philosophy na discoveries mpya kuhusu mwenendo wa mwanamke karibuni kila siku.

Utaamini wewe ni mwanaume mwenye mikosi na balaa na mkeo ni changamoto na tena source ya furaha yako hivyo hautaelewa namna ya kuishi nae na mwishoni upate maradhi ufe.

Ukichagua kuwaelewa wanawake then utashangaa sana kuona inakuwaje kuna watu wanaoa na kuwaweka ndani na kuwafanya watu wao wakaribu kushinda hata ndugu zao au wazazi wao. Utaelewa namna akili ya mwanamke inawaza na matokeo ya matendo yake bila kutumia akili nyingi. Hautaweza kaa na wanaume walio oa kwasababu kwa hoja zao wakikushangaa na wewe utawashangaa vile vile na kuwaonyesha waliposhikwa vibaya na hata wakikuelewa watakuogopa ama kukukwepa sababu ya hofu ya kuyaona yale ambayo walichagua kutoyaona au kujifunza juu ya mwanamke.

Kimsingi kama mtoto wa kiume jaribu kujitazama upo wapi, chagua upande ili usije pasuka kichwa kwa kushindwa kuelewa. Kuna wenzako wamewaelewa wanawake ndipo wakaoa kwa kuchagua toleo analoweza kuendana nalo. Halafu kuna wale wakaoa wakiwa hawana wanalojua kumhusu mwanamke wakajajikuta baadae wameshaingia mtegoni wakabakiwa na option ya kupenda tu kwa kanuni ya mapenzi ni upofu na kufunika kombe mwanaharamu apite.
 
Kweli kabisa
 
🀣Ila hii wiki umekamia wanawake...okay let's be friendly...wat happened to u.
Maana nyuzi ya nne cjui hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…