Ni aina gani ya Bima ya Afya anatumia Prof J (Joseph Haule)

Ni aina gani ya Bima ya Afya anatumia Prof J (Joseph Haule)

unprejudiced

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2017
Posts
3,503
Reaction score
2,865
Prof J ni moja ya watu maarufu kwa Level zetu za Tanzania. Pamoja na kuwa mbali na nyumbani kwa zaidi ya miaka 11 Lakini bado napenda kusikiliza Radio especially Clouds na Leo nimeskia kuwa Prof J ni mgonjwa na zaidi ya Wiki 3 amelazwa Hospitalini, gharama kwa Wiki 4 Million Tshs. Sio ndogo.

Swali langu kwa wenzetu mnaoishi na kutibiwa Muhimbili, je wanapokea Bima ya afya na wapi ni kikomo cha huduma Kadiri ya Bima ya afya. Je, Katika mazingira haya ya 4 Millionen per week, inawezekana kweli Prof anatumia Bima ya afya?

Imagine kwa mtu maskini na askofu yejulikana. Atafanyaje kupata 4 m kwa Wiki. Mwisho tuendelee kumwombea Jabali Prof J na michango Pia imwagike. Ingependaza michango ya aina Hii ingekwenda kwenye mfuko wa afya wa Bwana Prof J na kama itakuwa kea Hela kubaki baada ya matibabu yake Basi ingetumika kuwasaidia wenzine waliolazwa na hawana msaada.
 
tatizo sio bima .hata marehemu ruge kwao kuwa na pesa na kusaga kuwa napesa ya kufa mtu mbona bakuri lilipita.kuna magonjwa mengine yakikupata ni kama mchwa kwenye pesa
Umeongea Point , Cha Msingi Ni Kumsaidia Ndugu aweze Recove
 
Hakuna bima Ya Afya Tanzania Itakulipia 4m kwa Wiki. NHIF wenyewe Wamefilisika Wanalipia Dialysis Laki 2 Sijui Bima Itamsaidia Admission Tuu sio Matibabu.
 
Hakuna bima Ya Afya Tanzania Itakulipia 4m kwa Wiki. NHIF wenyewe Wamefilisika Wanalipia Dialysis Laki 2 Sijui Bima Itamsaidia Admission Tuu sio Matibabu.
angekuwa bado yupo mjengoni wale package yao imeshiba sio kama hizi za kawaida.

ina cover karibu kila kitu, wana package special ya bunge wanakatwa hela zaidi tofauti na watumishi wa serikali wengine.
 
unahis nini kwani? kuna magonjwa mengine hayatumii bima mkuu.

usipende kudodosa sana toa hela
 
Hakuna bima Ya Afya Tanzania Itakulipia 4m kwa Wiki. NHIF wenyewe Wamefilisika Wanalipia Dialysis Laki 2 Sijui Bima Itamsaidia Admission Tuu sio Matibabu.
Moja ya kitu nakiheshimu sana ni NHIF.
Nilimkatia mtoto ile TOTO AFYA KADI tu ila gharama ya operations ambazo imecover nisingemudu hata kidogo.
 
Tumsaidie prof jizze lakini suala hili la bima ni muhimu sana japo sio kila huduma ya afya inaweza lipiqa na NHIF labda mashirika mengine ya bima ya kimataifa ila huko nasikia package zake sio mchezo zinataka mtonyo mrefu sana
 
Hakuna bima Ya Afya Tanzania Itakulipia 4m kwa Wiki. NHIF wenyewe Wamefilisika Wanalipia Dialysis Laki 2 Sijui Bima Itamsaidia Admission Tuu sio Matibabu.
NHIF imefilisika kwa ujinga wake wenyewe baada ya kuanzisha bima ya wanafunzi kwa Tsh.50,400 ambayo ni sawa na bure kabisa ambampo huyo mwanafunzi anajikuta anatumia matibabu kama ya milioni kwa mwaka

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Hii ni kweli, kuna baadhi ya matibabu na dawa hazipo kwenye bima.
ndio

ingekuwa inatumia bima

basi figo zikifeli dawa yake kubadilishiwa figo nzuri.

kwa akili yako unahisi figo hiyo utaipata kwa pesa za bima yako? alokwambia nani?

magonjwa mengine km cancer n.k

watu wanahisi ukiwa na bima umemaliza kila kitu upande wa afya kumbe sio.
 
Moja ya kitu nakiheshimu sana ni NHIF.
Nilimkatia mtoto ile TOTO AFYA KADI tu ila gharama ya operations ambazo imecover nisingemudu hata kidogo.

Huyo yupo kwenye Package ambayo Haina Masharti Angalia bima Ya Mtu mzima, Mtoto unamkatia leo na ndani ya mwaka anaweza kufanya vitu vingi ila Adult ni mpaka bima iwe matured after 1 year na sahizi masharti yakuwa magumu kwasababu hawana hela na watoa huduma hawati kupata hasara. Ukiwa Mzima huezi elewa usumbufu wa NHIF na Hasa ukiwa na Magonjwa Chronic kama Kisukari, Pressure, kansa Na Mengine. Ukiumwa Malaria na UTI NHIF utaipenda
 
Back
Top Bottom