tatizo siku hizi kila mtu ni mtaalamu wa lishe, sasa kama na asali mnasema ni sumu mwilini, kimbilio [QUOTE="
Hakuna aliyesema Asali ni sumu...muulizaji alitaka kujua aina ya sukari yenye madhara..
Ndo tukasema katika mwili sukari ni sukari iwe ya kwenye soda, vitumbua, wali, chai au hata matunda vyote hv ni sukari ingawaje kwa matunda ni kuwa pamoja ya sukari mwili unapata vitamin.
Labda nikufafanulie kidogo tu..unapokula tuseme matuda...chakula kinakwenda kwenye tumbo (intestine)hapa usagwa, na kuna aina nyingi tu za Enzyme ambazo kuja kubebea aina mbalimbali ya vitamin na kupeleka sehemu inapotakiwa..Sasa basi katika hizo Enzyme zipo nyingine ambazo kazi yake ni kuchukua sukari (tuda ulilokula lina sukari) na kuibadilisha kuwa glucose...Hii glucose upelekwe kwenye damu, ikishafika kwenye damu usafirishwa tena kupelekwa katika sehemu mbali mbali ya mwili kwa ajiri ya energy , Mfn kwenye Muscles,.kichwani na nk..
Hivyo basi hawa Enzyme hawaangalii kama hii ni sukari inatoka kwenye wali, au.chai au matuda..wao sukari ni sukari...
Tatizo linakuja kama sukari ikiwa nyingi kwenye damu kuna kitu kinaitwa pancreas, hii pancreas ina produce kitu kinachoitwa Insulin (homon) hii homon kazi yake ni kupunguza sukari (glucose) iliyozidi kwenye damu yako, na kuibadilisha kuwa mafuta na kuhifadhi. Mafuta yakihifadhiwa na yakawa mengi matokeo ni unene..Madhara ya unene natunmaini unayafahamu
Nafikiri hapo utakuwa umeelewa ni kwa ninj tunasema sukari ni sukari