Ni aina ipi ya sukari isiyo na madhara mwilini?

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Naomba msaada wa kujua ni aina ipi ya sukari isiyo na madhara mwilini

1. Sukari iliyochemshwa kwenye chai ikachemka sana,

2. Sukari nyeupee iliyo korogwa kwenye chai papo hapo na ikanyweka,

3. Sukari Nyeupe iliyochemshwa kwenye chai ikachemka sana.

Mwenye jibu sahihi atujuze
 
sukari ni sumu inayo kumaliza kidogoo kidogo ila kama unatumia sukari fanya na mazoezi sana sio kwenda gym hapana penda kutembea sana kwa miguu yaani siku ukiweza kutembea 25000 steps hadi 30000 steps itasaidia magonjwa mengi utayapunguza lakini sukari sio nzuri
 
Sukari,asali, sukari guru zote zina same effects, tofauti ni kuwa nyingine ni fast reales.

Tumia sweeteners au cut off sugar kama una mashaka.
 
Sukari,asali, sukari guru zote zina same effects, tofauti ni kuwa nyingine ni fast reales.

Tumia sweeteners au cut off sugar kama una mashaka.
...Sky, Sijakuelewa. So wanatuaminisha kuwa Asali haina madhara sana na kama ukiweza kunywa cha kwa asali kuliko chain kwa sukari, maana Asali haina madhara ?? [emoji848][emoji848]
 
...Sky, Sijakuelewa. So wanatuaminisha kuwa Asali haina madhara sana na kama ukiweza kunywa cha kwa asali kuliko chain kwa sukari, maana Asali haina madhara ?? [emoji848][emoji848]
Asali ni monosaccharides inaenda mwilini faster lakini zaidi hapo zote ni sugar
 
Sukari,asali, sukari guru zote zina same effects, tofauti ni kuwa nyingine ni fast reales.

Tumia sweeteners au cut off sugar kama una mashaka.

Picha ya hizo sukari ulizotaja
 
tatizo siku hizi kila mtu ni mtaalamu wa lishe, sasa kama na asali mnasema ni sumu mwilini, kimbilio letu ni nini?

msitudanganye
 
Sukari ni sukari tu..iwe nyeupe, nyeusi, matunda au Asali zote ni sukari tu...
Sukari isiyo na madhara labda ni sweetener??...

Lakini sukari si sumu kama mnavyoaminishwa bali ni muhimu sana mwilini..Tatizo ukila sukari nyingi ndo ugekuwa kuwa si afya tena bali usababisha unene ambao mwisho ni magonjwa mbali mbali...Kama mtu huna ugonjwa wa kisukari na unatumia sukari kiasi ni sawa kwa mwili.
 
Kwa hiyo unashauri tutumie sweeter ile inayotumiwa na wagonjwa wa sukari sio
 
Kwa hiyo unashauri tutumie sweeter ile inayotumiwa na wagonjwa wa sukari sio
Tumia sukari ya kawaida lakini u..Kila kitu kikizidi uwa sumu..Sukari ni muhimu mwilini..

Kama nilivyosema sukari isiyozidi kipimo sio sumu..Sukari ni muhimu kwa kwani ina produce energy...Na energy ndo ufanya wewe ufikiri, unaposimama, tembea, kila movement unayofanya inatokana na energy..Energy inatokana glucose, glucose inatokana na sukari. Binadamu hawezi ishi bila glucose..
Hivyo sukari ikituma kwa kiwango cha kawaida haina madhara labda kwa mtu wa kisukari..Sweetener sina utalaamu n siwezi. Zielezea sana.
 
Kwa hiyo unashauri tutumie sweeter ile inayotumiwa na wagonjwa wa sukari sio

Unakuta unatumia hiyo sweetener then daily unapiga bia 5,6,7 n.k. Hiyo ndio huitwa kujitekenya mwenyewe kisha ucheke mwenyewe.

Mnapoambiwa sukari ni mbaya kwa afya haimaanishi ile sukari tunayotumia kwenye chai tuu mkuu.

Kuupa mwili sukari nyingi ndio hatari inayozungumziwa. Na source za kuingiza sukari mwilini ni nyingi sio kupitia chai tuu, hata ukila wali,ugali, tambi pia zote hizo ni source za sukari. Ukinywa soda, juice, bia pia ni source za sukari mwilini.

Hivyo kinachoshauriwa ni kupunguza kula vyakula vinavyoongeza kiwango cha sukari mwilini ila sio kupunguza ulaji wa ile sukari ya chai.

Nadhan mpaka hapo umepata picha kamili ilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…