Ni bahati au mafanikio ya TFF ya Karia

HPAUL

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2011
Posts
410
Reaction score
567
Tangu uongozi wa TFF chini ya Karia uingie madarakani Agosti 2017, kumekuwa na kawimbi ka mafanikio kiasi katika soka la Tanzania angalau kwa kiwango fulani kulinganisha na TFF za Malinzi na Tenga au hata FAT huko nyuma.

Mafanikio

1. Kuimarika kwa team ya under 17 ya akina Kelvin ambapo iliweza ku-qualify kushiriki fainali ya mwaka 2019.
2. Tanzania kwa mara ya kwanza iliweza kundaa fainali michezo Africa Under 17 mwaka 2019.
3. Baada ya miaka 37 Tanzania iliweza ku qualify fainali ya AFCON mwaka 2019 iliyofanyika Misri.
4, Kwa mara ya kwanza Tanzania katika ngazi ya klabu iliweza kuvuka hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika na kuingia robo fainali 2019 (wengi watasema hayo ni mafanikio ya juhudi binafsi za klabu ya Simba, lakini huko nje wanajua ni mafanikio ya Tanzania).
5. Tumeweza kuunda timu ya Under 20 imara Ngorongoro Heroes na kufanikiwa kuchukuwa kombe la Afrika Mashariki na ya kati ugenini 2019.
6. Baada ya miaka 10 Tanzania imefanikiwa tena ku-qualify kwa mashindano ya CHAN itakayofanyika Kameruni 2020.

Je, hayo ni mafanikio ya TFF ya Karia au ni upepo tu wa bahati? Na kama ni mafanikio, je kuna dalili yatakuwa endelevu? Naomba maoni yenu.
 
Hakuna cha bahati, bali angalau tumeona juhudi za Karia pamoja na kukosa fungu la kutosha kutoka serikalini. Kiukweli anahitaji pongezi za kutosha.
 
Uongozi bora kabisa kuwahi kutokea chini kwenye football Karia
 
Siyo bahati ni mikakati, mipangilio mingine kaikuta ila ameiboresha. Karia anastahili pongezi; tusimkatishe tamaa.

Namuomba Karia aboreshe academy za mpira na shule zenye programu za mpira, ikiwezekana atoe ruzuku kuziwezesha na kuziongeza.

Waziri Dkt. Mwakyembe pia apeleke mswada (agenda) bungeni ili kuongeza budget ya michezo kitaifa, tukitilia maanani mpira wa miguu!!
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Ni viongozi wengi wamepita na hatukuwahi hata kutoka kuwa kichwa cha mwendawazimu kuwa hata kichwa cha mlevi.

Licha ya mapungufu mengi katika uongozi wa Karia, bora hata katutoa kutoka kichwa cha mwendawazimu tumesogea hata kuwa kama kichwa cha mlevi. Japo bado tunayumba ila tukiacha pombe tukatulia na kuacha kuyumba tunaweza songa zaidi ya hapo tulipofikia. Hongera Karia pamoja na wasaidizi wako wote waliyo nyuma yako.
 
Naomba nikusahihishe.

U-17 haiku qualify CAN U17 2019 bali ilipita kwa mgongo wa wenyeji wa mashindano.

U-17 ilianza kuwa vizuri enzi za kina Mkomola, Dickson Job, hawa ndiyo wali-qualify CAN 2016 Gabon.

Mpira wa Tanzania ulibadilika toka enzi kocha Mbrazil.
 
Ni uongozi wa sasa TFF chini ya mwenyekiti Karia. Mwenyekiti si mtendaji sana lazima pale TFF kuna masterminds pembeni. Nchi kuonekana kwenye mashindano ya kimataifa mara kwa mara ni mafanikio. CHAN si michuano midogo pia.
 
Haya uliyoandika ni matokeo yaliyopatikana wakati TFF ikiwa chini ya Karia. Je unaweza ukatuorodheshea mikakati, na mipango iliyowekwa na TFF ya Karia ili kutengeneza hayo mafanikio tunayoyaona hapo juu? Ili tuone kama kuna jitihada zingine zilizofanyika tofauti na uongozi ziliyopita kuleta hayo matokeo au imetokea tu kibahati
 
Ikifuzu kombe la dunia, nitaipongeza TFF. Ila kwa matokeo ya jana, naweza kusema ni bahati tu iliangukia upande wa timu yetu . Zaidi labda ni kuwapongeza wachezaji kwa kupambana kwao mwanzi mwisho, hata baada ya kuwa nyuma kwa magoli mawili!
 
Bahati tuu, jamaa wameunda kamati yao ambayo itakua inatoa viongozi tuu, hawana jipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…