Nakushauri usikope fedha na upeleka kwenye kilimo.
Sababu za kukuambia hivyo ziko nyingi kati ya hizo Ni:-
a) Hatuna Sera nzuri zinazosimamia kilimo, nikiwa na maana hii, viongozi wenye dhamana muda wowote wanasema chochote, kama kuzuia mazao kuuzwa nje ya nchi.
b) Kati ya sekta zinazoadhiriwa na mabadiliko ya Tabia nchi Ni kilimo, hii inamaana risk ni kubwa kwenye kilimo.
c) Nguvu ya soko, katika nchi yetu bei ya bidhaa inabadilika mno kukiwa na sababu za ndani na nje(internal and external factors) mfano zao LA nyanya mwezi wa sita box moja la kilo 25 liliuzwa tsh 45000, mwezi mmoja baadae box hilohilo liliuzwa tsh 8000. mwezi wa nane limeuzwa 2000mwanzoni na baadae zikaanza kuozea shambani.
Kama unataka kujikita kwenye kilimo fuata ushauri uliopewa wa kuanza kidogo kidogo ili kujifunza changamoto zilizopo eneo husika.
Asante