That's True coz hakuna kitu tamu kama mkopoHakuna kitu mbaya kama pesa ya mkopo kuitumia kuanzisha project ni mbaya sana mkuu bt pesa ya mkopo hutumika kukuza project na hapa ndipo watumishi wengi walokimbilia bank huanza kujuta
my take! anza kilimo hata kwa nusu ekari kwa kutumia mshahara wako then baadae kupitia zao hilo hilo utakuwa ushajua abc zake ingia bank komba pesa kawekeze
all the best
Ni kweli kabisa MkuuWanakudanganya Mkuu
hata aliyekupa wazo kuwa ukalime matikiti maji.
wewe upo latila ajira ya serikali na unataka uende kijijini ukalime mpunga na matukutu maji.
UNALO SOKO????
mbona uanataka hiyo pesa ikukate na uibiwe
halafu uje JF na mrejesho wa kilio
nakushauri km huna kz nazo achana na mpango
Zingatia ushauri wangu utakusaidia:
Usikope kwenda kuanzisha biashara kwa kua biashara inachangamoto nyingi, kopa kwaajili ya kuboresha biashara kwa kua utakua na uzoefu na unazijua changamoto za hiyo biashara na kuwa na uhakika wa kupata faida na kurejesha.
Watoa ushauri walio wengi hawakuambii changamoto za hicho wanacho kushauri na kukupigia hesabu rahisi na kukuaminisha kuwa kuna super profit .
Huwezi kukua bila ya kukopaNakushauri usikope fedha na upeleka kwenye kilimo.
Sababu za kukuambia hivyo ziko nyingi kati ya hizo Ni:-
a) Hatuna Sera nzuri zinazosimamia kilimo, nikiwa na maana hii, viongozi wenye dhamana muda wowote wanasema chochote, kama kuzuia mazao kuuzwa nje ya nchi.
b) Kati ya sekta zinazoadhiriwa na mabadiliko ya Tabia nchi Ni kilimo, hii inamaana risk ni kubwa kwenye kilimo.
c) Nguvu ya soko, katika nchi yetu bei ya bidhaa inabadilika mno kukiwa na sababu za ndani na nje(internal and external factors) mfano zao LA nyanya mwezi wa sita box moja la kilo 25 liliuzwa tsh 45000, mwezi mmoja baadae box hilohilo liliuzwa tsh 8000. mwezi wa nane limeuzwa 2000mwanzoni na baadae zikaanza kuozea shambani.
Kama unataka kujikita kwenye kilimo fuata ushauri uliopewa wa kuanza kidogo kidogo ili kujifunza changamoto zilizopo eneo husika.
Asante
Nakushauri usikope kwanza anza kilimo kwa mtaji mdogo kwanza ambao utatoka ktk mshahara wako.Heshima kwenu.
Mimi ni mwajiliwa wa serikali na mwezi huu natimiza mwaka mmoja.
Niko kijijini na kuna fursa kubwa ya kilimo cha mpunga na tikiti maji so nimeamua kulima kilimo cha kisasa.
Nataka nikope walau m13 kutoka benki za NMB au CRDB kwani ndo zipo maeneo ya karibu.
Hivyo basi wadau, naomba ushauri wapi pa kukopa kwa riba nafuu bila ya usumbufu wa kuombwa rushwa.
Natanguliza shukrani.
NB: Mshahara wangu ni D kwa viwango vya serikali.
hawa jamaa riba yao ni kubwa me naoona wako poa ni equity ile ya kenya ila huko cdhani kama ipo crdb na nmb bora nmb ila kaka kweli m13 ukalime tikiti? asee labda ungenambia ununue mashamba na viwanja ukae baada ya miezi 6 unauzaunanunua tena au ununue mashamba upande miti isisahau kuwa na mradi ambao utakufanya ile gap ya mshahara usiione me nina kiduka kidogo kinansogeza na nlinunua viwanja so nasubiria mwakani nianze kuviuza nijengeTanzania Postal Bank ( TPB ) hutojuta!!