Ni biashara/huduma ipi unaweza kufanya/kutoa ambayo haina bei elekezi?

Ni biashara/huduma ipi unaweza kufanya/kutoa ambayo haina bei elekezi?

kimara Kimara

Member
Joined
Jul 7, 2024
Posts
80
Reaction score
173
Habari wadau, moja kwa moja kwenye mada.

Ni biashara gani ama huduma ipi unaweza kufanya ambayo haina BEI ELEKEZI, yani bei unajipangia wewe mwenyewe?

Mfano wa biashara za bei elekezi nin kama duka la takataka, Madawa, Vyakula, Kuuza magari, nguo, nafaka n.k.
Naomba kujua biashara/ huduma ambazo unaweza fanya na hazina bei elekezi.
 
Kuchoma dawa wanyama majumbani.
Kuuza kitimoto.
Udalali magari.
KUuza simu used
Kuuza nguo za dukani
 
Sehemu ambayo nilipigia hela NI hapa...kufungua ballo za mitumba....ujue kuuza...narudia ujue kuuza....hakuna Bei elekezi....biashara za computer kusaidia watu kuapply au kuitengeneza doc mbalimbali...hazina Bei elekezi zipo nyingi ukishaingia field nyingi huwa deal garama au hazipo rasmi watakufunza wateja waliona unaziweka....
 
Msaada kiongozi ballo za nguo aina gani zinauzika zaidi?
 
Bidhaa nyingi zinapangia bei na soko, bei ya jumla na madalali hata kama zina bei elekezi. Mfano unaweza kuta leo bei ya viazi sokoni ni 75,000 lakini kesho kutwa vikafika 100,000 kutokana na soko la siku hiyo. Pia madalali bidhaa inauzwa 5000 wao wanasema 9000. Kama unauza kwa reja reja pia inategemea umenunua bei gn kwa jumla, same product at the same location lakini Bei tofauti.We chagua biashara unayotaka kuifanya tafuta waliokutangulia wakufundishe game linavyoenda
 
Back
Top Bottom