GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kuna Mtu nimepishana nae akiwa katika Harrier matata sana huku akiwa na Mikogo yote (kama ya Watani zangu Wakubwa Wahaya) cha Kushangaza baada ya Nusu Saa nimekutana nae Ubungo anapakia Magunia ya Pumba za Kuku huku akiwa Kavua Shati kutokana na Joto Kali la Dar es Salaam sasa (ambalo TMA hawajatuambia bado linatokana na nini) pembeni yake Taita (Tajiiri na mwenye Gari) anamsimamia huku akimfokea kwa Kuyapanga vibaya hayo Magunia.
Mpaka sasa najiuliza Maswali mengi mno tu kwa ile Mikogo yake ( ambayo natamani Ningeirekodi ili nanyi muone) hakuna ambaye angeamini kuwa kumbe Yeye ni Dereva tu ( siyo Mmiliki ) na kwamba alikuwa anawahi Kubeba Magunia ya Pumba ya Boss wake kwa ajili ya Kupelekea Kuku Bandani Kwake.
Na nahisi huyu Dereva atakuwa Mhaya.