Ni dalili gani zinazoonesha unatumika?

Lakini pia mtu anaweza kukutumia kama daraja la kuvuka Kisha akakutupa huko.

Sifa zao: Hawa ni watu wenye mbinu za hali ya juu, wenye hila, na wanaoangalia maslahi yao binafsi pekee (self-interest).

Mienendo yao: Hawatazami mahusiano au urafiki kama kiungo cha kihisia, bali kama nyenzo au mtaji (utility) wa kuwasaidia kufika wanapotaka. Wakishapata walichokuwa wanakitafuta (iwe ni fedha, hadhi, connection, au mtaji), thamani ya lile "daraja" (wewe) inaisha, na hapo ndipo wanapokutupa bila majonzi.
 
Umeongea vizuri mkuu asante sana
 
Full stop..

Cha kuongezea tu

Kwenye maisha bora uwe unatumika kwa sababu inaonesha una thamani flani kuliko kuwa useless. Ila sasa ni kuhakikisha unapotumika na wewe panakufaidisha maana kutumika ni lazma, haiepukiki

Ukijiajiri utatumika, ukiajiriwa utatumika. Ukiingia kwenye mahusiano utatumika, ukitaka show time utatumika.
Ukisaidia watu pasipo malipo utatumika, na hata ukiwalipisha bado utatumika.

Haiepukiki kwa sababu binadamu hajitoshelezi kwa mahitaji yake wala haridhiki kiakili, kihisia na kiroho bila mchango wa mtu mwingine. Tunaishi kwa kutegemeana na ndio kutumiana kwenyewe
 

Mkuu nadhani umechanganya dhana mbili tofauti hapa, kutumiana na kutumika.

Hoja yako ingekuwa sahihi kama kila anayetoa mchango angekuwa anapata haki yake lakini dunia imejaa mifano ya watu waliodanganywa, wakatumia muda, fedha na nguvu zao kwa ahadi za uongo.

Kutumika ni pale ambapo upande mmoja tu ndiyo unapata faida Mkuu.
 
Mtu huyu pia anaangukia kwenye kundi la wale ambao wanatafuta matunda ya mafanikio lakini hawataki kuvumilia changamoto za safari.


Mkakati wao: Ni watafuta fursa (Opportunist) Wanakuja kwako kwa sababu umeonyesha uwezo, nidhamu, au una rasilimali fulani ambayo wao hawana (daraja la kuvukia).


Uthibitisho wa Tabia: Wana utatuzi wa haraka wa matatizo yao lakini wana upungufu mkubwa wa uaminifu wa muda mrefu (long-term loyalty) na ukosefu wa ukomavu wa tabia (character integrity).

Mtazamo wa Kimkakati (The Strategic Takeaway)

Mtu wa namna hii anathibitisha kile alichosema Mchungaji Rose Shaboka:
"ubaya wao unatokana na jinsi walivyo ndani yao, na si kwa sababu wewe ulikosea wakati unamsaidia."
 

Full stop..

Cha kuongezea tu

Kwenye maisha bora uwe unatumika kwa sababu inaonesha una thamani flani kuliko kuwa useless. Ila sasa ni kuhakikisha unapotumika na wewe panakufaidisha maana kutumika ni lazma, haiepukiki
Huamini kama kuna watu wanatumiwa au wanatumika for nothing ?
Hapa anazungumiziwa mtu anaetumika kwa ulaghai kwa kudanganywa wala hafaidiki chochote au faida ni kiduchu mnoo
 
Mada nzuri sana, KUTUMIKA iwe kwenye ajira, mahusiano, urafiki, ndoa ni kawaida na wengi wanatumika bila kujua kama wanatumika.

Unafanya kazi ambayo mshahara unaopata na kile unachompa boss wako haviendani, hukwo ni kutumika. Ukifikia retirement age wanakunyali na kukuweka pembeni as if hukuwa na mchango wowote kwao.

Upo na rafiki yako, yeye anakutafuta akiwa na changamoto tu, yaani akiwa oky wala humsikii, akiwa na shida ya buku 50 anakutafuta, ukimsaidia hutamsikia tena, hata ukimtafuta wewe hana time, unatumika.

Upo na mkaka, yeye anakutafuta akiwa na shida ya ngono tu, yaani akiwa hana nyege hutamsikia, ila kibubu kikijaa chaap sana. Likewise upo na mdada, yeye akiwa na shida zake za vikoba ndio anakutafuta, ukishatatua shida zake hata uhangaike vipi hutamsikia, atakukwepa kama ukoma.

Huko kwenye ndoa ndio usiseme, watu wanatumika sana, sio kwa faida ya familia, bali mke au mume.
 
Umeuliza dalili Shesrise
Wacha mimi niseme kwenye relnship
Nafsi huugua sana, you will feel drained instead of being energized every time you interact with the peeson,Internal conflict inside you will be so vivid and loud.
 
Huamini kama kuna watu wanatumiwa au wanatumika for nothing ?

Hapa anazungumiziwa mtu anaetumika kwa ulaghai kwa kudanganywa wala hafaidiki chochote au faida ni kiduchu mnoo
Ndio maana nikasisitiza ukitumika hakikisha unanufaika kwa sababu kutumika bila kukunufaisha ndio unapopaita "kutumika".

Yani unafanyiwa dhulma ila wewe unaichukulia kawaida kwa sababu, pengine una moyo mzuri, unajichukulia poa, hujui thamani halisi ya kitu unachokifanya au kuna ule uoga unaotokana na kuzoea routine flani kwa hiyo unaona, nikiiacha hii kazi, hii connection, nikimuacha huyu mtu. Ni nini kitatokea au nitaishije

Kutumika kwa asili ya neno lake ni kitendo cha watu kuitumia usefullness yako. Ila pale watu wanapoitumia pasipo kukufaidisha ndio tunaita "manipulation" Au kulaghaiwa.

Sikutaka kuongelea hili but kiufupi, hii dunia kutumika hakuepukiki ila kulaghaiwa kama unavyosema. Kunaepukika
 
Kupiga miayo mara kwa mara,ni moja wapo ya dalili ya kutumiwa ama kutumika pia.
 
Asante babu yangu mzurii🥰
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…