Ni dhahiri kuwa awamu ya tano haikuwa sikivu kusiliza ushauri wa Mawawaziri, ilipobainika hivyo waliamua kufunika kombe

Ni dhahiri kuwa awamu ya tano haikuwa sikivu kusiliza ushauri wa Mawawaziri, ilipobainika hivyo waliamua kufunika kombe

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Ibara ya 54(2) imetanabaisha wazi kuwa baraza la mawaziri ndio kitakuwa chombo kikuu cha kutoa ushauri kwa rais ili aweze kutekeleza majukumu yake.

Hata kabla ya kumaliza maombolezo tangu afariki hayati Dkt. John Pombe Magufuli tunasikia kauli za kushangaza toka kwa baadhi ya waliokuwa mawaziri chini ya utawala aliouongoza. Na hawa mawaziri walikuwa ni wajumbe wa baraza la mawaziri. Mfano ni Nape Nnauye anadiliki kusema kulikuwa na mapungufu juu ya kusimamia haki za binadamu. Huku mwingine akidai kuwa kama mtaalamu wa tiba kujifukiza hakusaidii kuzuia Covid 19.

Mbali na hayo pia suala la kutumia mitutu ya bunduki kukusanya kodi kupitia task force pia linatia doa awamu iliyopita na sasa tunaona kama limezuiwa mapema kabisa.

Hivyo tunapata picha kabisa kumbe baadhi ya mawaziri waliotumikia awamu ya tano walikuwa wanaona dosari nyingi zikifanyika ila kwa kuona kuwa watawala hawashauriki basi waliamua kukaa kimya japokuwa kwa kinafiki ili mkate upatikane.

N.B Makamu wa rais pia ni mjumbe wa baraza la Mawaziri.
 
Nk sawa tu na kuhoji mapato na matumizi Chadema.
 
Ahaaa, mkuu lini alijisifia?

Kwenye ule uzi wako namba1 usiseme watawala walikuwa hawashauriki, sema Magufuli ndio alikuwa hashauriki, maana hakustahili kuwa rais, na hakuwa na uwezo wa cheo cha urais.
 
Kwenye ule uzi wako namba1 usiseme watawala walikuwa hawashauriki, sema Magufuli ndio alikuwa hashauriki, maana hakustahili kuwa rais, na hakuwa na uwezo wa cheo cha urais.
Mkuu kumbuka kwenye cabinet yupo rais, makamu wa rais na waziri mkuu.
 
Back
Top Bottom