Huu uzi haujapata wachangiaji wengi, kwakua consumers wengi wa burudani ya mziki siku hizi hawafwatilii DJs sana. Wanadownload nyimbo mitandaoni na kucheck youtube tu,tofauti na zamani lazima usikilize vipindi vikali vya radio na television ndiyo upate burudani. So lazima utakuwa unawajuwa DJs ata zaidi ya kumi.
Djs bora kabisa kwa upande wangu mwaka huu ni hawa;
DJ Polepole a.k.a "Slowslow" huyu anapigia (sukuma gang)
DJ Nape huyu anapigia (wenyewe ndiyo sisi)
DJ Mbowe huyu anaupiga mwingi sana pamoja na kupita kwenye matatizo lakini amekuwa akipiga mapambio huko huko, huyu anapigia (ufipa club)
DJ ndugai huyu ana mixing za hatari za kushangaza hadi kituo anacho pigia wanajua lolote linaweza kutoke, hasa akishika mike kufanya hype, huyu anapigia (lumumba club).