Ni faida au hasara kama mwanafunzi watalipa nauli za wakubwa kwenye daladala?

Ni faida au hasara kama mwanafunzi watalipa nauli za wakubwa kwenye daladala?

fikramoto

Member
Joined
Dec 9, 2014
Posts
7
Reaction score
2
Endapo wanafunzi watalipa nauli za wakubwa kwenye dala-dala, mojawapo ya faida ni kwamba: HAWATA ACHWA KABISA VITUONI NA USAFIRI WAO UTAKUWA NI WA UHAKIKA.

Je upande wa HASARA ni nini? Kama itaonekana faida ni kubwa kuliko hasara nashauri Serikali itangaze nauli moja kwa wote bila kujali mwanafunzi.

Ni wazo nimewakilisha.
 
Hasara ni gharama kubwa kwa wazazi,say nina watoto wanne wanasafiri kila siku kila mtoto anatumia sh 800 mara watoto 4 napata 3200 na kwa mwezi napata 256,000/=.

Mkuu hii pesa ni kubwa kwa mtanzania mwenye kipato cha kawaida na watanzania wengi wanafall humu

Nadhani tuhamasike tu kusomesha watoto wetu jirani na maskani ili kuepusha hizi gharama na kuepusha hatari zinazoweza kuwapata wakati wa kusafiri
 
Mkuu Mi Nadhan Utofaut Wa Naul Kati Ya Mtoto Na Mt Mzima Lazma Uwepo,haiwezekan Mtoto Asie Na Chanz Cha Mapato Alipe Sawa Na Mjasiriamali,,tena Me Nashaur Serikali Iondoe Kabsa Nauli Kw Wanafunz Coz Kwny Daladala Hawathaminiw Ingawa Wanalpa Hy Mia2
 
Back
Top Bottom