Ni fikra za umaskini zinazofanya watu wafikiri kila aliyefanikiwa ni freemason ama atoa kafara au chuki dhidi ya waliofanikiwa?

Ni fikra za umaskini zinazofanya watu wafikiri kila aliyefanikiwa ni freemason ama atoa kafara au chuki dhidi ya waliofanikiwa?

Manzile

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2020
Posts
701
Reaction score
1,900
Habari zenu ndugu zangu.

Kuna mambo Huwa nashindwa kuyaelewa.

Watanzania tumekuwa na kasumba za ajabu, Umaskini wa baadhi umetufanya tuwe na roho mbaya, chuki, husda Kwa waliofanikiwa bila hata sababu ya msingi.

Nimeshuhudia na kusikia hadithi za watu wengi waliofanikiwa sehemu ninazoishi kutoka Kwa watu wasiofanikiwa asilimia kubwa Huwa ni uongo na chuki binafsi.

Mawazo ya mtanzania yanawaza kila aliyefanikiwa ni mtoa kafara ama freemason, tena kama ametoka familia ya kimaskini bahati ikawa upande wake akafanikiwe, kelele zitakuwa kila kona mpaka Kwa ndugu zake akituhumiwa uchawi.

Hizi fikra zitatuisha lini?
Hivi ni kweli tunajiaminisha jamii zetu haziwezi kufanikiwa bila uchawi?

Kwa Nini tunakuwa na chuki, husda na roho mbaya Kwa wenzetu waliotuzidi kimaisha? Sababu Huwa ni hasa?

Unawezaje kumchukia mtu kisa tu kafanikiwa kuliko wewe?

Kuna mambo yanashangaza kwenye hii Dunia
 
Matajiri ni wachawi tofaufi ya maskini na tajiri nini?? Yeye ametengenezewa akafanikiwa yule hajafanikiwa basi ndo ananyea nyea
 
usiombee ndo mtu afariki ghafla nakuamby ndugu zako Wataacha kupokea ela zako michango yako aisee na vikao vya sili vitakuwa vingi sana kukujadili mwamba
 
Hakuna mafanikio marahisi mdogo wangu, iwe ni real hustle au kafara zote ni njia hii dunia ina siri nyingi nzito sana ambazo mimi na wewe hatuzijui.
 
usiombee ndo mtu afariki ghafla nakuamby ndugu zako Wataacha kupokea ela zako michango yako aisee na vikao vya sili vitakuwa vingi sana kukujadili mwamba
Haha
 
Siku hizi wamepata sababu nyingine pia,mtu akifanikiwa na hasa akiwa kijana,utasikia wakisema Shoga yule!

Kama uchawi unaleta utajiri,basi na wewe kafanye huo uchawi ili na wewe uwe tajiri.
 
Siku hizi wamepata sababu nyingine pia,mtu akifanikiwa na hasa akiwa kijana,utasikia wakisema Shoga yule!

Kama uchawi unaleta utajiri,basi na wewe kafanye huo uchawi ili na wewe uwe tajiri.
Ni chuki za kijinga za watu weusi ndio maana hatuendelei
 
Back
Top Bottom