Elections 2010 Ni haki mbwa kuvalishwa tisheti ya Kikwete?

RMA

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2010
Posts
409
Reaction score
87
Polisi huko Songea wanamtafuta mtoto wa darasa la Sita kwa kumvisha mbwa tisheti ya CCM. Hata watoto wamechoshwa na CCM. Huyo mtoto asisumbuliwe. Ameonyesha uzalendo wake. Watanzania wote waige mfano. Popote pale mbwa walipo wakamatwe, wapewe zawadi za CCM dakika hizi za lala salama.
 
 
Hii inaonesha kabisa siasa za Tanzania ni za KIDINI. Huyu mtoto katumwa na Vigogo fulani, ili wamtukane KIKWETE kwa sababu ni muislamu. Ktk, Mbwa ni Najisi kubwa.
Waislamu watafanya juu na chini kuhakikisha huyu PADRE Slaa haongozi nchi.
 
hapana jamani, mtu mwanamume akimpa mkeo nguo si ana kudharau? Tena nguo yenye picha yake? Ndio maana huyo mwanamume akaone bora akamvalishe mbwa ili kujibu dharau. Hata akimpa mtoto wako nguo huku mwanao huyo hawezi kula vizuri, hapati elimu nzuri, si dharau hiyo pia? Hawa CCM kama wana hela kiasi hicho si wangeboresha shule au dispensari ya hapo kijijini, wangepata wapi presha wanayoipata au matusi wanayopewa sasa?
 
Anaonyesha mtazamo wake Jamani!!!
 
Mimi nitawavalisha kunguru wooote Dar Skafu za Kiwetee... Oppss Kikwete...
 
Wewe ndo mdini kwani umeambiwa Dr Slaa anagombea upadri? Ongea labda sera zake ni mbaya or Else, othrerwise huna mpya.
 
Kwani shida iko wapi kumvika mbwa gauni au nguo ya aina yoyote? Check hizi picha za mbwa na tishet ya Obama. Kama obama anvaliwa na mbwa who is Kikwete?
View attachment 15805View attachment 15806


Problem ni kwamba hawa polisi wetu hawajui sheria na ndio wanapenda kunyanyasa wananchi. Mfano ya polisi kupiga watu walio kwisha kukubali arrest. That is wrong and things need to change! POLISI ACHENI KUNYANYASA WATANZANIA KWA UJINGA WENU. We are free people as long atuvunji sheria.
 
amefanya la maana mi sioni kosa la yule mtoto
 
[QOUTE]nitzschiller
Junior Member

Join Date
Wed Oct 2010
Posts
1
Thanks
0
Thanked 0 Times in 0 PostsRep Power
0
[/QUOTE] Karibu mkuu, au ni id ya pili?
 

.
Tulishughudia hawa mahakimu wa kwetu wakisaidiwa na afande mwendesha mashitaka kumhukumu mbwa kifo, kisa ati mwenyenae kampa jina la immigration. Labda sisi weusi tujitahidi kujikoboa kwa mkorogo huenda huu weupe wa kununua ukazifanya akili zetu nazo kukaribia kufanana na za weupe(wazungu).
 
mtoto wa darasa la sita, Juhudi zetu zinalipa, moyo wa mageusi na mabadiliko inaingua ndani ya rika stahili, tUnawekeza kwa hao watoto, asante Tanzania, asanteni nyoote....msichome moto nguo zao, wapeni mbwa na nguruwe wavae ........
 
Hii inaonesha kabisa siasa za Tanzania ni za KIDINI. Huyu mtoto katumwa na Vigogo fulani, ili wamtukane KIKWETE kwa sababu ni muislamu. Ktk, Mbwa ni Najisi kubwa.
Waislamu watafanya juu na chini kuhakikisha huyu PADRE Slaa haongozi nchi.
Hapana, wewe una lako jambo, si lazima ishu za udini zije hapa
 
jamani hizo fulana zimetengenezwa kwa pesa ya kodi yetu huyo mtoto ameangalia matatizo yake akaona hayajaangaliwa badala yake anapewa tisheti ambayo si hitaji lake,angeweza kuichoma moto lakini kwa busara akaona afikishe ujumbe kwa kikwete kwa na mbwa nao ni watz labda ndio aliowalenga kwa kuwa hitaji la mtz wakawaida sio hilo.huyu mtoto apelekwe shule ya vipaji maalum kwa kuwa imaelekea ubongo wake si wa kawaida.anatafakari kabla ya kuchukua hatua.na wote wanaoipenda nchi hii kila atakaeiona tisheti ya ccm afikishe ujumbe si lazima kumvalisha mbwa kwa sababu itakuwa sawa na kuchungulia mtihani,kila mtu atumie akili yake. habari ndiyo hiyo.
 
Duhh! Naomba vyama vya kiraia kumtetea huyo mtoto. Fulana ya kikwete si nguo za kuvaliwa ila ni bango la matangazo kwa mjibu wa sheria za uchaguzi. Sioni kosa mbwa kuwekewa bango hilo maana anapeleka ujumbe kwa watu wengi kuliko namna nyingine. Naomba wanasheria wamtetee mtoto huyu. Mimi niko tayari kutoa mchango wa kifedha. Naomba tuwasiliane na wanasheria wa taasisi za kijamii ili tumtetee mtoto huyu maana hana kosa!!!:A S angry:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…