Ni halali Hakimu kufungua kesi ya jinai pasipo kupitia Polisi?

Wambugani

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2007
Posts
1,757
Reaction score
277
Nimeona mara nyingi mahakimu wa Mahakama ya Mwanzo Karatu kufungua kesi za Jinai pasipo malalamiko au mashtaka kupitia polisi. Je, wadau utaratibu huu ni halali kisheria na katika kesi hizo washitakiwa wamekuwa wakinyimwa hata fursa za kujitetea na kwa vile kesi inachukua muda mrefu washitakiwa wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu kwa kufika Mahakamani pasipo kusikilizwa ama kuonewa kwa kesi kama hizo ambazo mara nyingi zinafunguliwa kwa ubabe.

Kesi hizo zinajenya mianya ya rushwa na uonevu kwa raia wasio na hatia,

Ninatumaini chini Serikali ya Rais John Maguguli na Waziri wa Sheria na Katiba, Mh. Harryson Mwakyembe, uonevu huu utakoma.
 
Nijibu swali lako la msingi malalamiko wapelekee wahusika.
Kesi za jinai zinafunguliwa mahakama za mwanzo kwa namna mbili:-
1. Kwa kupokea hati ya mashitaka kutoka polisi
2.kwa kupokea malalamiko moja kwa moja kutoka kwa mlalamikaji.
 
uko sahihi
 
Kama zitafunguliwa moja kwa moja Mahakamani huo sio mradi wa Mahakimu?
 
Nimeona mara nyingi mahakimu wa Mahakama ya Mwanzo Karatu kufungua kesi za Jinai pasipo malalamiko au mashtaka kupitia polisi. Je, wadau utaratibu huu ni halali kisheria na katika kesi hizo washitakiwa wamekuwa wakinyimwa hata fursa za kujitetea na kwa vile kesi inachukua muda mrefu washitakiwa wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu kwa kufika Mahakamani pasipo kusikilizwa ama kuonewa kwa kesi kama hizo ambazo mara nyingi zinafunguliwa kwa ubabe.

Kesi hizo zinajenya mianya ya rushwa na uonevu kwa raia wasio na hatia,

Ninatumaini chini Serikali ya Rais John Maguguli na Waziri wa Sheria na Katiba, Mh. Harryson Mwakyembe, uonevu huu utakoma.

kwanza kabisa hakimu hafungui kesi. na huo utaratibu upo.

pili mtu yoyote anaweza akafungua kesi ya jinai katika mahakama ya mwanzo kwa yale makosa tu ya jinai ambayo yana uwezo wa kusikilizwa na mahakama ya mwanzo pasipo kupitia polisi (sio lazima) japo pia anaweza kupitia polisi.

tatu mahakama ya mwanzo haina proper au specified document katika kufungua kesi ya jinai kama ilivyo katika mahakama zingine ambapo charge sheet hutumika katika kufungua kesi za jinai.
 
Back
Top Bottom