mimi sio mshabiki wa uchawi. Ila swala la mtu na mungu wake ni binafsi. Mimi namwamini Mungu wa mbinguni, na siwezi kumlaumu mtu anaye amini wachawi, majini (yani mashetani). Kazi yangu (na yako) ni kumpa ushaidi kwamba Mungu wangu ndo Mungu wa ukweli. Ila kwasababu na sisi tunaojifanya kwamba tuna Mungu wa ukweli lakini matendo yetu na tabia zetu ni kama wao, wenzetu wanashindwa kuelewa Mungu wetu na miungu yao ina tofauti gani. kazi yangu na kazi yako ni kuwathibitishia wanaoamini uchawi kwamba Mungu wa Mbinguni ndo Mungu peke wa kuabudu, au sivyo lets not make noise at them when we havent settled our relationship with our God. Na kibaya zaidi, wote mbele za Mungu sote ni wadhambi hakuna aliye na upper hand.