msnajo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 3,066
- 1,141
Ndg zangu naomba kuwasilisha hii mada. Kwa kifupi ni kwamba kuna jamaa yangu ana gf wake na wamekua kwenye mahusiano kwa muda wa 3 yrs. Mwaka jana Oct yule gf ali-conceive, baada ya miezi 2 kwa bahati mbaya ikatokea miscarriage. Kaka yake yule gf akashtuka na kuanza kumlaum yule jamaa yangu kuwa wameshirikiana kufanya abortion. Ilikuwa mzozo ila daktari ndie aliokoa. Walikaa kikao wakajadili kuwa jamaa atamchukua gf kutoka kwao lini, jamaa akaomba apewe muda wa miezi 2 ili awashirikishe wazazi na ndg zake ili ikiwezekana afanye mchakato wa mipango ya vikao. Kabla ya miez 2 kuisha yule gf akamwambia jamaa yangu kuwa anataka ahamie kwake hakuna haja ya kusubiri hiyo miez 2 iishe. Yule jamaa akamkatalia na wakakwaruzana kwa swala lile. Wakiwa kwenye mkwaruzano yule gf akaja kwa nguvu na cku jamaa anarudi ucku kuhangaika anamkuta gf wake yupo nyumban anasema haondoki tena coz alikua na funguo nae pia. Yule bwana alinitext nikamuuliza, ameaga kwao? Akasema hapana na hawajui alipo. Nikachakachua nikamsihi amweleze Kakake gf ili isilete shda. Kaka akafoka sana kuwa hatambui anachotaka ni taarifa kuwa dadake keshaolewa. Yalikuwa makubwa sana coz yule gf alimkwaza jamaa kwa kitendo cha kuja kuhamia kwa nguvu, akimlazimisha amuoe na kumfokea kama mtoto. Alifikia mahali akampiga yule jamaa na cm ikamuumiza mdomo wa juu na kuvuja damu! Ilinckitisha sana. Jamaa akasema, ok, kwa kuwa ameamua kuja kwa nguvu na ujeuri akaamua kusepa na kumwacha gf nyumbani na cm imezimwa, so hapatikani ila kwa watu wachache. Nlishauri aripot police ili kaka yake gf asijesema mdogo wake ametoroshwa. Tuliripot coz yule gf alimwambia yule jamaa atajiua na kumuua yeye. Nikachunguza kwa makini sana nikagundua kuwa yule gf alilazimishwa na kakake na wifi yake kuwa aondoke home, cjui alikuwa anawakwaza nini? Mbaya zaidi aliekua anatoa shinikizo la kumwondoa nyumban ni wifi yake. Mpaka hapa ninapoandika hi mada yule jamaa ameapa hatomrudia yule bint ila nina wasiwasi kwani mapenzi ni mdudu wa ajabu sana. Yule bnt kwa kuwa aliona miez 2 ni ming sana sasa ana wakati mgumu na anamlaum kakake na wifi kwa kuwa lengo halikutimia! Kaka ke nae ana hasira coz huenda akamkosa shemeji mwenye chapaa.. Ushauri wangu ni kuwa pamoja na kwamba tunawapenda sana wake zetu, tuangalie na kupima ushauri wao, na pia mdogo wangu wa kuzaliwa inakuwaje namlazimishe kwenda kuolewa!. This is true story, naomba mchakato wa mawazo ili tumwongezee jamaa yangu ushauri. Na je akiamua kumrudia yule gf atumie taratibu zipi kuhakikisha hatopigwa tena na cm au kuropokewa kama ilivyokuwa hivi majuzi. Natanguliza shukrani zangu wakuu.