GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Mimi siyo mfuasi wa Chama Chochote cha siasa, ila ni mpiga kuta mwaminifu. Sichagui Chama, namchagua mtu.
Msigwa ni mwanachama wa CCM kwa sasa. Lakini miezi michache iliyopita, alikuwa CHADEMA akiwa ni mmoja wa viongozi waandamizi wa hicho chama.
Baada ya kuhamia CCM, amegeuka kuwa mmoja wa wakosaoaji wakubwa wa CHADEMA, Chama alichokitumikia kwa zaidi ya miaka kumi.
Japo ni kawaida wanasiasa kukosoa vyama hasimu, naona kama Msigwa anakosea kuikosoa CHADEMA. Ukosoaji wake unaweza kumpunguzua credits toka kwa wapiga kura.
1. Angeweza kuonekana ana hoja kama angekuwa ameondoka angali na wadhifa. Kitendo cha yeye kuondoka baada ya kukosa uwennyekiti wa Kanda kutaleta tafsiri kuwa anakosoa kwa kuwa alikosa madaraka
2. Kahamia CCM kwa kuwa kaona kuwa ni Chama kizuri kuzidi CHADEMA. Lakini CCM bado haijarekebisha mambo ambayo wana CHADEMA walikuwa wakiyalalamikia kwa muda mrefu. Msimamo wake kwa sasa utabadilika au naye sasa atakuwa miongoni mwa watu watakaokuwa wakituhumiwa na vyama vya upinzani?
Kwa mfano:
A. Wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA walioingizwa bungeni kibabe kinyume cha Katiba
B. Manung'uniko kuwa CCM huwa inaiba kura kama ilivyotukia mwaka 2020
C. CCM kuhusishwa na kuwanunua viongozi wa vyama vya upinzani hasa CHADEMA
Japo mimi si mtaalam wa Siasa, lakini naona kuwa ni bora Msigwa angeepuka kuikosoa CHADEMA kwa sasa kwani kufanya hivyo ni kujiabisha.
Angeiga mfano wa hayati Edward Lowassa na Mh. Lazaro Nyalandu.
Lowassa alipoenda CHADEMA, hakuiporomoshea CCM matusi. Na hata aliporejea CCM, alifunga kinywa chake dhidi ya CHADEMA.
Hata Nyalandu naye, baada ya kurudi CCM, hakuanzisha vita na CHADEMA.
Msigwa naye anaweza kujijengea heshima kisiasa bila kukituhumu Chama kilichomlea.