Ni Harusi ipi ( gani ) inayonoga zaidi na ndiyo inatakiwa kwa Maisha ya sasa ( Magunu na Nafuu ) kati ya hizi Mbili zifuatazo?

Ni Harusi ipi ( gani ) inayonoga zaidi na ndiyo inatakiwa kwa Maisha ya sasa ( Magunu na Nafuu ) kati ya hizi Mbili zifuatazo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
A. Ya Kuoa / Kuolewa kwa Kuomba ( Kupitisha ) Michango kwa Watu na bado wakija Ukumbuni Bia za Kulazimisha kupewa, Soda za Kuvizia na Chakula cha Kukadiriwa na hapo hapo bado unatakiwa ukawawazawadie wana Ndoa Meza Kuu?

B. Ya Kuoa / Kuolewa kwa Wanandoa Kujichanga Wenyewe kwa kila Kitu huku nyie Wageni ( Marafiki ) mkialikwa Kuhudhuria ambapo Vinywaji vyote na Vyakula vilivyopo Mezani Ukumbuni ni halali yako na hata Kutoa Zawadi kwa Wanandoa ni Hiari yako.

Majibu yenu hapa yanaweza Kunishawishi nami GENTAMYCINE nianze sasa Kufikiria Kuoa nikifikisha Miaka 50 au 55 kwani kwa sasa Msamiati wa Kuoa bado haupo Ubongoni mwangu kwakuwa kwa Wanawake waliopo sijaona wa Kuwaoa ( Kuoa ) kutokana na 'Changamoto' zao tukuka.
 
A. Ya Kuoa / Kuolewa kwa Kuomba ( Kupitisha ) Michango kwa Watu na bado wakija Ukumbuni Bia za Kulazimisha kupewa, Soda za Kuvizia na Chakula cha Kukadiriwa na hapo hapo bado unatakiwa ukawawazawadie wana Ndoa Meza Kuu?
B
 
Unaonekana unapenda sana 'Slope' Mkuu. Na katika huu huu Uzi leo nitawajua wale wapenda Kuteleza ( Kitonga ), Wabahili wa Kuchangia Harusi na Wazee wa 'Kuzamia' Harusi za Watu ( Wenzao )
 
Nachagua
A.
---
Ufafanuzi
  • Hata kama una uwezo wa kifedha haipaswi kutoshirikisha ndugu jamaa na marafiki kukuchangia.
  • Angalia huu mfano wa shilingi: Harusi(sherehe) ni upande mmoja wa shilingi katika maisha yetu, Na upande wapili wa shilingi ni Kifo(huzuni) pale unapofiwa, Hakika utahitaji ndugu na jamaa wakufariji kwa upande huu wa pili wa shilingi katika maisha, haijalishi u_tajiri kwa kiasi gani ukifikwa, lazima utahitaji ndugu jamaa na rafiki wakufariji na kukusaidia kumpumzisha mpedwa wako.

Hitimisho.
bado wakija Ukumbuni Bia za Kulazimisha kupewa, Soda za Kuvizia na Chakula cha Kukadiriwa na hapo hapo bado
Kwa wahusika wa sherehe, wawe wanajipanga vyema kimahesabu, ili kuondoa au kupunguza hii changamoto ya vinywaji/Chakula
 
Harusi nzuri yafaa wahusika wajipange wenyewe, sisi waalikwa tutafika na chochote kitu ili kuwazawadia…. sio ile michango ya lazima.
 
Nachagua
A.
---
Ufafanuzi
  • Hata kama una uwezo wa kifedha haipaswi kutoshirikisha ndugu jamaa na marafiki kukuchangia.
  • Angalia huu mfano wa shilingi: Harusi(sherehe) ni upande mmoja wa shilingi katika maisha yetu, Na upande wapili wa shilingi ni Kifo(huzuni) pale unapofiwa, Hakika utahitaji ndugu na jamaa wakufariji kwa upande huu wa pili wa shilingi katika maisha, haijalishi u_tajiri kwa kiasi gani ukifikwa, lazima utahitaji ndugu jamaa na rafiki wakufariji na kukusaidia kumpumzisha mpedwa wako.

Hitimisho.

Kwa wahusika wa sherehe, wawe wanajipanga vyema kimahesabu, ili kuondoa au kupunguza hii changamoto ya vinywaji/Chakula

Ila asilimia kubwa ya wasiojiweza wanategemea michango kama ndiyo base ya kusimama harusi,unapoanzisha jambo au umepanga harusi uwe na bajeti yako wewe au kama nyinyi wahusika.michango si lazima au kulazimishana kudaiana kila siku,Ni uamuzi wa mtu kuchangia au kutochangia,na fungu la michango nyinyi kama nyinyi msiliweke kama muhimu sana kiasi ambacho kama hakitapatikana kile kiasi ambacho mnakitaka ratiba itabadilika munatakiwa michango iwe tu kama pesa ya nyongeza ipo kama itatokea kuongezea chochote tu.Ubaya ni ule wa kusema sihitaji mchango wa mtu utaonekana mbinafsi.Harusi kama harusi uzuri wa kuchangiwa ni muhimu hata kama una uwezo kama kuonesha ushirikiano uliousema hapo juu.Tatizo zama hizi weengi wanakuwa wanatumia michango ndiyo kama bajeti kubwa ya harusi ikiwa hatafika kiwango chao walichokikadiria wanakuwa wamevurugwa na malengo yao, sasa kama wangekaa wao kama wao sisi tuna bajeti hii ya harusi kwa pesa zetu kama ni mkopo unakadiria kama milioni 10 kama mfano tu.Hujaingiza mchango hapo wakachanga ukapata labda milioni tano.unakuwa una 15 ila lengo lako ni 10 ifanyike sasa tano zitakusaidia kwa mambo ya maisha huko mnapoelekea.lakini siyo ili ifanyike inahitaji milioni 5 wahusika muna milioni moja tu kwa hili lazima mutawakera watu na kila siku kuulizana michango.
 
Back
Top Bottom