Ni hatua gani nifuate ili kuonana na Rais?

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Nina shauri langu la ardhi lakini naona linapindishwa waziwazi hakika sina pa kukimbilia sina wa kumlilia naona nitadhulumika waziwazi.

Ni dhuluma za kipuuzi kabisa ardhi pameoza workers are not for customers or listening or do for normal clients.

Naomba taratibu za kumuona Rais nimechoka kwelikweli.
 
Kumuona Rais Bongo ni connection, usidhani ni Sugu binafsi ndio alifanikiwa kumualika Rais kwenye concert lake na akahudhuria, kuna watu wapo nyuma ya camera wanafanikisha haya.

Mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa kila wiki wana siku moja ya kusikiliza wananchi ofisini kwao na hawa ndio wawakilishi wa Rais, anza na hawa.

Kama umeshapita kote huko ndio ujitowe akili sasa andaa bango lako vizia siku Rais ana mkutano wa hadhara unaliamsha dude utasikilizwa.

Ila kama hujapita kwa Dc na Rc nakushauri pita huko, mimi binafsi Sophia Mjema alipokuwa Dc ilala alimaliza issue yangu ya ardhi kwa kupiga simu tu kitengo cha ardhi kwa kina Lugano.

Tanzania viongozi wa kisiasa wateule wa Rais wana nguvu kubwa kuliko unavyofikiri na wanaogopwa na hao watumishi wanaobabaisha watu.
 
Inshallaalh
 
jizoe na ujikusanye pruuuuuuuuu mpaka geti jeupe.

utaruhusiwa ila lazima uingie ofisi ya mapokezi kwa mkurugenzi wa itifaki ikulu pale pale getini,shida ya pale hutapewa mualiko kama swala lako linatatulika na mamlaka za chini huku,ndio maama wenzako huwa wanaparamia mike kwenye misafara,ingawa siku hizi hakuna tena misafara ya wananachi ya ana kwa ana.

kajaribu bahati yako bana unawezashinikiza ukapelekewa kwa waziri wa ardhi.
 
Fuata ngazi kwa kuanzia mjumbe wa shina wa chaka chako.....
 
Nina shauri langu la ardhi lakini naona linapindishwa waziwazi hakika sina pa kukimbilia sina wa kumlilia naona nitadhulumika waziwazi.

Ni dhuluma za kipuuzi kabisa ardhi pameoza workers are not for customers or listening or do for normal clients.

Naomba taratibu za kumuona Rais nimechoka kwelikweli.
Unawaza kuonana na mh rais wewe njoo hapa JF na documents zote oandisha Uzi wataje wahusika wote mod akifuta wewe unapandisha akifuta unapandisha uone ndani ya siku wiki tu jambo lako litakuwa solved njoo andika afisa aridhi....... Acha dhuruma uone uko ofisini watakavyotafutana na kuforwadiana
 
Mbona kwa rais ni mbali?
Jitahidi tu uonane na naibu waziri wa ardhi. Ni kijana mchapakazi, kijana wa dot.com Hana longo longo au njaa za kuomba rushwa.
 
Back
Top Bottom