Ni hatua ipi ulifikia ya madhara hadi ikawa hamasa yako kuachana na uraibu au mazoea potevu uliyokuwa nayo??

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Nilikuaga mpenzi sana wa soda aina ya coca cola iliyo ya baridi sana.

Ilikuwa siku ikiisha bila kupiga coca najiona mtupu.

Matter of fact ingebidi nipatiwe tuzo ya mnywaji bora coz nilikuwa nakunywa kila siku.

Hadi hapo siku moja nilianza kuhisi meno yangu ya mbele kuanza kuuma pale napokunywa kitu cha baridi, moto au chenye sukari sana (kitamu sana)

Nilipotezea, ila hali ilianza kuwa mbaya ikawa sasa nikiyagusa hata kidogo hata na hewa ya baridi yanauma hadi kupelekea kupata headache ya siku nzima.

Na maumivu haya yalikuwa yanatesa vibaya sana.

Ndipo nilipofanya utafiti nikajua nina pitia shida inaitwa "SENSITIVE TOOTH".

Ndipo nika google namna ya kuindoa nikaona recomendations ya dawa za meno zilizo special kwa ajili ya sensitivity ya jino, ilinigharimu 15,000 dawa moja na inapaswa nitumia karibia wiki 7 ili ukae vizuri kabisa.

Ila pia inatakiwa uache matumizi ya carbobated drinks, citrus, vitu baridi sana.

Naendelea vizur kwa sasa na Tangia nimepitia maumivu yale ya jino aisee sitaki tena coca cola.
 
Matumizi ya pombe kali bila kula. Ilikuwa kila siku hasubui mpaka usiku kabla ya kulala Kvant kubwa tatu lazima ziishe. Nikapoteza mpaka appetite ya msosi baada ya miaka mitatu nikakonda nikaanza kubanduka ngozi ya mikono kwenye viganga na miguu, kutembea ikawa shida. Kwenda kwenye hospitali zetu huku kagera wakasema damu ni chafu nikapewa dozi nikarudi nyumbani kabla sijaanza dozi nikasema ngoja ninywe ka mwisho mwisho aisee nilizidiwa nikapelekwa hospitali usiku wakanilaza tumia dawa kalibia wiki mbili sioni dalili nikasema cha kufia nn nikakimbilia benjamini mkapa hospital wale jamaa wanamachine kama zote. Baada ya vipimo vyote wakaniuliza kama natumbia pombe kali nikakwambia hapa ndo nyumbani kwao basi wakanipa vidonge na tube za kupaka kumbe nilikuwa naumwa fungus miezi miwili nikawa fresh nikaludisha majeshi nyumbani. Toka siku vinywaji vigumu no.
 
Dalili za mtu anayetaka kuunda NGO akawapige wafadhili
 
Hamna siku ilikuwa inapita bila kahawa au energy drink aisee. Yaani ndio siku yangu inakuwa nzuri naweza kufanya shughuli zangu. Mezani kwangu vitu hivi vilikuwa havikosi. Nilikuja kuacha nilipokuwa na ujauzito wa kwanza. Sikurudia tena mpaka sasa, miaka karibia 10 imepita sasa sitamani kabisa kuwa tegemezi wa caffeine tena
 
Sasa ule usemi wa "kenge hasikii hadi atoke damu sikioni" ndiyo ulitimia kwako.

Ungeendelea kuwa mbishi,sasa hivi jua lingekuwa linawaka juu ya kaburi lako.

Hongera.
 
Duh pole mkuu

Hongera pia
 
Ilikupa madhara yoyote yale??
 
Sasa ule usemi wa "kenge hasikii hadi atoke damu sikioni" ndiyo ulitimia kwako.

Ungeendelea kuwa mbishi,sasa hivi jua lingekuwa linawaka juu ya kaburi lako.

Hongera.
Duu kwa kwwl
 
Ilikupa madhara yoyote yale??
Mbali na kunichangamsha 😂 Mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda mbio kama unataka kuchomoka na kupungua uzito maana ilikuwa inaleta hali ya kutosikia njaa. Nilikuwa tegemezi kwa kipindi kirefu miaka 8 kabla ya kuachana nayo kabisa
 
Hahaha hongera lakin
 
Hahaha hongera lakin
Nilianza na kahawa baadae nikaona haifui dafu kwa energy drink 🤣 na hautaamini, lakini sijui ni nini kinawekwa kwenye mo na azam energy maana zenyewe unakuwa na cheche yaani unawaka tofauti na imports kama red bull au monster 😂😂
 
Back
Top Bottom