Ni hatua zipi muhimu za mtu hupitia hadi kujinasibu kuwa yeye ni shabiki wa timu fulani?

mzee wa kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
947
Reaction score
685
Ninajiuliza swali. Ni hatua zipi muhimu za mtu hupitia Hadi kujinasibu kuwa yeye ni shabiki Wa timu fulani?

2.Je kuna Kosa gani kwa shabiki Huyo kuamua Kubadili gear angani na kujiunga na timu nzuri ya msimu husika?

3.Kocha anahama timu, wachezaji unaowapenda wote wanahama wewe unashabikia nini?
4.Ushabiki Wa kizamani unakufanya ufe na timu moja

5.Ushabiki Wa kisasa,chagua timu Mwanzo Wa msimu angalia usajili angalia kocha jihakikishie furaha kwa mwaka mzima

6. Sii Kosa shabiki kuwa na timu mbili hata tatu ndani ya nchi moja mfano,mm msimu ujao kwa Tanzânia Nitakuwa shabiki Wa Yanga na Singida united.

Uingereza Nitakuwa Man U na Chelsea
Spain Nipo Madrid
Kombe lá Dunia Brazil na UK
Unaona nimejihakikishia raha mwaka mzima sina presha

Wewe baki na Katimu kako kamoja kanakupa pressa huna raha. Njoo kwenye ushabiki Wa kisasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni rahisi kubadili mke kuliko kubadili timu unayoishabikia.
 
Ni makosa makubwa kwa mwanaume kuwa na mke mmoja au mwanamke kuwa na mume bila hawara
 
Kichwa cha habari na comments za humu ndani tofauti kabisa
 
Wewe hata kwenye maisha yako utakuwa unatangatanga. Akili ikiwa ni iliyotulia na kujielewa basi ni kila sehemu hata mchezoni.

Me, Myself and I
 
Umeandika kichwa cha habari kana kwamba unataka upate majibu kutoka kwa wachangiaji ila ndani ya thread unajiuliza na kujijibu mwenyewe

anyway inabidi ujue kuwa kuna shabiki na mshangiliaji, unachoongelea wewe ni ushangiliaji, unaweza kushangilia team yoyote ile bila sababu ya msingi kwa wakati fulani na badae unaweza kushangilia team ingine tena

Ushabiki waga hauji tu from no where, ushabiki ni from heart, ni hisia na ndomana huwezi kuja kuona mfano eti Liverpool kisa haijashinda makombe muda mrefu mashabiki wapungue uwanjani hiyo haipo na ndio kwanza wanaongezeka, ushabiki ungekuwa hivo basi kila mtu angeshabikia Barcelona, real Madrid, man u na leo hii team km Ac milan zingekuwa hazina mashabiki

Mara nyingi unakuta mchezaji anacheza zaidi ya team 5 ila kuna team moja ndo inakuwa moyoni mwake na kuipa heshima ya nyumbani, kwa mchezaji mpira unabaki kazi ila ushabiki pia una nafasi yake

mfano Henry kacheza monaco, juventus, Arsenal, Barcelona ila club iliyopo moyoni mwake ni Arsenal
Mfano tena rooney kacheza man u kwa mafanikio makubwa sana na kapata heshima kubwa pale man u ila club iliyopo moyoni ni Everton kwani ndio ambayo anaisapoti tangu utotoni

So jifunze kwanza kutofautisha ushangiliaji na ushabiki then siku ingine utaandika uzi wenye mantiki na sio huu utoto wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilimchukua muda gani Huyo shabiki kuamua kuwa shabiki Wa hiyo timu? Na kwanini hawezi kuhama?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilimchukua muda gani Huyo shabiki kuamua kuwa shabiki Wa hiyo timu? Na kwanini hawezi kuhama?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa shabiki wa team wala haikuchukui muda kama vile unatafuta mke...! Mara nyingi hutokea tu kama accidentally, sometimes hutokea siku unaangalia mpira labda siku ya marudio, na match zinakuwa nyingi, itapita man u, itapita Chelsea, itapita Liverpool, itafika Newcastle unahisi tu kutoka moyoni kuwa kuna kitu umekipenda kuhusu Newcastle, so ikitokea ukaitazama mara 2, 3 unaona hisia zinazidi kukua kila uionapo

Na ili ujue kuwa wewe ni shabiki wa team fulani, utakuwa unapenda sana kuona inashinda, na ikifungwa unaumia sana, huo ndio ushabiki

So haina haja ya kujiandaa kabisa eti naanza kutafuta team ya kushabikia, hutokea tu kama ile wazungu wanaita love at the first sight. ila kushangilia unaweza anza na Netherlands katika world Cup, ikitoka, unaenda Germany, ikitoka unaenda Hispania nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachokufanya usipende timu nyingine au usiachane na Mapenzi ya Mwanzo ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…