mwananchi01
New Member
- Aug 20, 2022
- 1
- 4
Binafsi nimekaa na kutafakari sana kuhusu Serikali yetu inapambana kuanzisha mifumo ya kielektroniki ili kurahisisha utoaji wa huduma zake. Mimi pia nimenufaika moja kwa moja kwa jitihada hizi maana napata/nalipia huduma za Serikali kwa njia rahisi sana huku nikiwa naendelea na shughuli zangu.
Mambo ya kwenda kwenye taasisi za serikali kupanga foleni ili kulipia huduma mbalimbali kama kodi ya ardhi, umeme, maji, n.k nimeshasahau kabisa. Napata bili zangu kwa USSD (*152*00#) au kwakutumia App ya GePG TANZANIA kirahisi kabisa.
Lakini inaonesha bado kuna taasisi chache ambao huduma wanazozitoa unaweza kuzipata bila kwenda kwenye taasisi hizo lakini kwa utaratibu wao wanalazimisha mpaka ufike ofisini ndiyo upatiwe huduma ambayo kwa mtazamo wangu haijakaa vizuri, maana inakupotezea muda na kukuongezea usumbufu bila sababu.
Taja taasisi ya Serikali ambayo inafaa iboreshe huduma zake ziendane na zama za sasa za Sayansi na Teknolojia.