SOMA HAPA:-
Dawa za maleria zipo nyingi nzuri na mbaya,kinachotakiwa ni mtu kuwa makini na mdadisi.
Kwa sasa kutokana na usugu wa malaria,unashauriwa kutumia dawa ambazo ni mchanganyiko(mseto) ingawa kuna baadhi ya watu dawa ambazo si mseto bado zinawatibu. Dawa ambazo ni mseto zilizo sokoni tanzania na maelezo yake ni kama ifuatavyo
1-Coartem-huu ni mchanganyiko wa dawa mbili(Artemether+Lumefantrine 20/120mg) Dawa hii inapendekezwa na wizara ya afya na ni nzuri kwa kweli kwani watu wengi(si wote) wanapona bila matatizo au kwa matatizo yanayovumilika. Tatizo lake ni vidonge vingi kwa dozi(24) pia ni kwamba mwanzoni ilikuwa inatengenezwa Switzerland lakini mchina kaaingia na anatengeneza under licence,unajua mambo yake, pili serikali ilipandisha kodi kwa kampuni binafsi za dawa kwa hiyo pamoja na kutoka china bado garama zake si chini ya Tsh 15000 kwa dozi,lakini hata hivyo serikali inazipata kutoka swiz kwa bei nafuu lakini kwa paki tofauti na za mwanzo(sijui ubora wake) huu ndo mseto au Alu za serikali
Tatu ni kwamba wahindi nao wameingia baada ya kuona mseto unatumika,unapendwa na ni ghali,kwa hiyo wamekuja na zao za bei rahisi(ubora sina uhakika) zenye majina ya biashara..Artefan,lumaterm,lumerax tena zenye vidonge vichache mfano (dozi vidonge 6 badala ya 24)
Watu wananunua buku 1 mpaka 2000,zinawasaidia ila hazijatumika muda mrefu sijui madhara yake ya muda mrefu(long term effect)
2-Duocotecxin (dihydroartemesinin+piperaquine 40/320mg) inatoka china,ni nzuri zaidi ya 70% ya watu wanatumia bila shida ila kwa wale isiyowafaa ina madhara makubwa kama kushusha presha na hata kuua(rare) Tatizo lake ni kwamba ukitumia iliyokaa,tuseme zaidi ya miaka miwili hata kama tarehe ya expire haijafika haiponeshi na ndo maana wamebadili idadi ya vidonge(zamani vilikuwa 8 dozi 3/3/2 siku hizi 9 dozi 9/9/9 kwa wakubwa) vinginevyoo si mbaya lakini ni ghali >Tsh10000 brand
3-Artequine(artesunate+mefloquine 600/750 etc) ni nzuri kwa watu wasio na matatizo ya moyo,lakini inasumbua kwa watajwa tena inaweza kufanya hali ikawa mbaya sana. Bei ni ghali pia>Tsh11000 lakini kama utaweza kununua ni nzuri tu kama huwezi mseto(ya dozi vidonge 24)
4-Ntaendelea kesho pita pita,umeme umekatika na betri yangu chaji imeisha ntaendelea