Naomba kujua dawa nzuri ya kutibu maji, hasa angavu kama ya mto, yafae kwa matumizi ya nyumbani kama kunywa, n.k. Pia naomba kujua ujazo, bei ya dawa husika, na madhara yake.
N.B. Nataka kutibu maji kama lita 80,0000
Karibu kwa mchango wako.
dawa nzuri inayotumika kutibu maji kabla kila mahali duniani ni 'chlorine', sidhani kama inauza kwenye maduka ya kawaida, ila nina uhakika nimeona galoni za lita 5 zenye chlorine zikisafirishwa kuelekea vijijini.
Jaribu kwenda idara ya maji iliyopo karibu ili wataalamu wakupe maelezo zaidi

Nimeongea na injinia mmoja wa idara ya maji, kama ulovyosema - chlorine haiuzwi kwenye maduka ya kawaida, wao wanauza nusu lita kwa sh. 25,000.
Hivyo nitaendelea na mpango wangu wa kujenga karo kubwa la maji ya mvua. Maji hayo yakiisha kabla ya masika nitaweka ya kutoa kwenye visima vya mkono au ya mtaro. Mita kadhaa kutoka nyumbani kuna mtaro huwa unatirisha maji kutoka kwenye chemchem karibia mwaka mzima