Ni ipi dawa ya kutibu mdondo kwa kuku?

Ni ipi dawa ya kutibu mdondo kwa kuku?

Husna Muba

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
14,524
Reaction score
44,577
Habari wakuu

Naomba mnusaidie kunielekeza dawa ya kutibu mdondo wa kuku. Naomba iwe ya kienyeji bandugu
 
Huo ugonjwa unatakiwa kuwakinga na si kuwatibu. Sana sana utakuwa unatibu side effects kama wameshambuliwa tayari ila kupona ni 50/50
 
Jani la alovera unakamua maji yake na kuwanywesha
Hapa atapata shida kufanya hilo zoezi la kukamua.
Njia rahisi, kata katia jani la alovera vipande vidogo kama vya chips katika maji yaliyopo kwenye chombo chaocha maji.
 
Magonjwa ya kuku ni hatari sana kwa wafugaji.
Mimi ninachokifanya, nachanganya madawa yote yaliyofanyiwa utafiti kuwa yanatibu magonjwa ya kuku. Baada ya kuyachanganya nakausha alafu nasaga kupata unga ambao nauchanganya kwenye chakula cha kuku alafu nawapatia kuku wangu. Hii imenisaidia kuondokana na changamoto hizo.
 
Good, nitajie na mimi hayo madawa nichanganyeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu

Naomba mnusaidie kunielekeza dawa ya kutibu mdondo wa kuku. Naomba iwe ya kienyeji bandugu

Mdondo hauna dawa. Unapaswa kuwachanja kuwakinga nao. Ukichelewa u r fucked big time.

Unaweza kuwapa alovera kama chanjo. Inasaidia sana.
 
Back
Top Bottom