Ni ipi faida ya Bima ya vyombo vya moto?

mbenda said

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2019
Posts
1,084
Reaction score
2,074
Habari wana zengo natumai wote ni wazima wa afya tele.

Mm naomba kufahamishwa faida ya bima ya vyombo vya moto hasa hii bima ndogo ambayo ni lazima kila chombo cha moto uwe nacho, mm naomba kujua nn faida ya huyu mmili wa chombo kama piki piki, bajaji na gali anapata faida gani akiwa nayo?
 
Bima ndogo faida ni kwa 3rd party.. yaani mtu utakaemletea madhara kwenye ajali.

Hata kama wewe ama mali yako huijali.. unapaswa uwajali wengine utakaowaletea madhara.. ndio maana sheria ya bima inakulazimisha uwe na 3rd party
 
Bado cjakuelewa mkuu, nn faida ya bima ndogo, yaani ninakata bima napata faida gani?
 
Yaani ni hivi kwa mfano unaendesha gari yako halafu ukamgonga mtembea kwa miguu na kumsababishia majeraha au ulemavu huyo mtu,hiyo bima ndiyo itakayomlipa yule mtu uliyemgonga kuhusu matibabu yake na fidia,na pia hata ukigonga chombo kingine kama gari,pikipiki ukawasababishia uharibifu kwenye hivyo vyombo bima ndio itawalipa hao wenye vyombo ulivyogonga.
Wewe uliyemgonga hautawajibika kumlipa yule mtu uliyemgonga hiyo ndio faida yake,ila wewe uliyesababisha ajali haulipwi hata kama gari yako imepata uharibifu.
Nadhani hapo umeelewa sasa

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Ni kwel lakn mbona hiyo bima haiwasidii walengwa?
 
Back
Top Bottom