Kila kitu kina faida na hasara zake, japo siwezi kukupa jibu la swali lako, lakini tambua mjasiriamali lazima awe "RISK TAKER" hivyo we jaribu tu utaona matokeo yake. Jambo la msingi ni kuhakikisha una weka biashara yako mahali penye soko, pia pasiwe penye competition kubwa, na uwe mbunifu zaidi. Utatoka tu ndugu yangu.
Lakini ukisema uulize faida utapewa majibu kulingana na mtu, mwingine kashindwa biashara mwenyewe basi ataponda tu, mwingine hajui lolote ila kwakuwa ana chuki zake na watu wa tigo basi ataponda tu. We tambua biashara ambayo unaona watu wanafanya kila siku hiyo ina faida, ila ni muhimu uwe na ufahamu wa biashara walau kidogo, iwe kwa kusoma darasni, au kwa ufahamu wa kawaida tu, au hata kufundishwa kwa namna yoyote itasaidia zaidi.